Mathayo 5
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
1耶稣看见这许多的人,就上了山,既已坐下,门徒到他跟前来,
2naye akaanza kuwafundisha:
2他就开口教训他们,说:
3“Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
3虚心的人有福了! 因为天国是他们的。
4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
4哀恸的人有福了! 因为他们必得安慰。
5Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
5温柔的人有福了! 因为他们必承受地土。
6Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
6饥渴慕义的人有福了! 因为他们必得饱足。
7Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
7怜恤人的人有福了! 因为他们必蒙怜恤。
8Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
8清心的人有福了! 因为他们必得见 神。
9Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
9使人和睦的人有福了! 因为他们必称为 神的儿子。
10Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
10为义受逼迫的人有福了! 因为天国是他们的。
11“Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
11「人若因我辱骂你们,逼迫你们,捏造各样坏话毁谤你们,你们就有福了!
12Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
12应当欢喜快乐,因为你们在天上的赏赐是大的。在你们以前的先知,人也是这样逼迫他们。」
13“Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
13「你们是世上的盐。盐若失了味,怎能叫它再咸呢?以后无用,不过丢在外面,被人践踏了。
14“Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
14你们是世上的光。城造在山上是不能隐藏的。
15Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
15人点灯,不放在斗底下,是放在灯台上,就照亮一家的人。
16Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”
16你们的光也当这样照在人前,叫他们看见你们的好行为,便将荣耀归给你们在天上的父。」
17“Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
17「莫想我来要废掉律法和先知。我来不是要废掉,乃是要成全。
18Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
18我实在告诉你们,就是到天地都废去了,律法的一点一画也不能废去,都要成全。
19Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
19所以,无论何人废掉这诫命中最小的一条,又教训人这样做,他在天国要称为最小的。但无论何人遵行这诫命,又教训人遵行,他在天国要称为大的。
20Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
20我告诉你们,你们的义若不胜于文士和法利赛人的义,断不能进天国。」
21“Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
21「你们听见有吩咐古人的话,说:『不可杀人』; 又说 :『凡杀人的难免受审判。』
22Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
22只是我告诉你们,凡向弟兄动怒的,难免受审断;凡骂弟兄是拉加的,难免公会 的审断 ;凡骂弟兄是魔利的,难免地狱的火。
23Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
23所以,你在祭坛上献礼物的时候,若想起弟兄向你怀怨,
24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
24就把礼物留在坛前,先去同弟兄和好,然后来献礼物。
25“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
25你同告你的对头还在路上,就赶紧与他和息,恐怕他把你送给审判官,审判官交付衙役,你就下在监里了。
26Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
26我实在告诉你,若有一文钱没有还清,你断不能从那里出来。」
27“Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
27「你们听见有话说:『不可奸淫。』
28Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
28只是我告诉你们,凡看见妇女就动淫念的,这人心里已经与她犯奸淫了。
29Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.
29若是你的右眼叫你跌倒,就剜出来丢掉,宁可失去百体中的一体,不叫全身丢在地狱里。
30Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.
30若是右手叫你跌倒,就砍下来丢掉,宁可失去百体中的一体,不叫全身下入地狱。」
31“Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
31「又有话说:『人若休妻,就当给她休书。』
32Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
32只是我告诉你们,凡休妻的,若不是为淫乱的缘故,就是叫她作淫妇了;人若娶这被休的妇人,也是犯奸淫了。」
33“Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
33「你们又听见有吩咐古人的话,说:『不可背誓,所起的誓总要向主谨守。』
34Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
34只是我告诉你们,什么誓都不可起。不可指着天起誓,因为天是 神的座位;
35wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
35不可指着地起誓,因为地是他的脚凳;也不可指着 耶路撒冷 起誓,因为 耶路撒冷 是大君的京城;
36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
36又不可指着你的头起誓,因为你不能使一根头发变黑变白了。
37Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
37你们的话,是,就说是;不是,就说不是;若再多说就是出于那恶者。」
38“Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
38「你们听见有话说:『以眼还眼,以牙还牙。』
39Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
39只是我告诉你们,不要与恶人作对。有人打你的右脸,连左脸也转过来由他打;
40Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
40有人想要告你,要拿你的里衣,连外衣也由他拿去;
41Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
41有人强逼你走一里路,你就同他走二里;
42Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.
42有求你的,就给他;有向你借贷的,不可推辞。」
43“Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
43「你们听见有话说:『当爱你的邻舍,恨你的仇敌。』
44Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi
44只是我告诉你们,要爱你们的仇敌,为那逼迫你们的祷告。
45ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
45这样 就可以作你们天父的儿子;因为他叫日头照好人,也照歹人;降雨给义人,也给不义的人。
46Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
46你们若 单 爱那爱你们的人,有什么赏赐呢?就是税吏不也是这样行吗?
47Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
47你们若单请你弟兄的安,比人有什么长处呢?就是外邦人不也是这样行吗?
48Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
48所以,你们要完全,像你们的天父完全一样。」
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.