Mathayo
Chapter 13
Biblia Takatifu (Swahili…

Read in

Smith–Van Dyck Arabic Bible (فان دايك)Brezhoneg (Breton Gospels, 1827)Judson Burmese Bible (1840)Chamorro: Gospels, Acts and PsalmsChinese Union Version, punctuated (Simplified)Chinese Union Version, punctuated (Traditional)Coptic New TestamentCoptic New Testament (Bohairic)Kralice Bible (1613)Testamenta Marra (Dieri New Testament)Petrus Canisius Bible, 1939 (De Heilige Schrift)Asang Khongca Bible (Eastern Khumi Chin, 2019)Berean Standard BibleDouay-Rheims Bible, American Edition (1899)King James Version with ApocryphaWorld English BibleLondona Biblio (Esperanto, 1910)Louis Segond 1910Lutherbibel 1912Greek New Testament, word by word (STEPBible TAGNT)Greek New Testament: 1904 Patriarchal Text (Byzantine)Greek New Testament: Byzantine Text (Robinson–Pierpont 2018)Greek New Testament: Textus ReceptusSBL Greek New TestamentBaibala Hemolele (Hawaiian Bible, 1868 revision)Modern Hebrew BibleDiodati Bibbia 1885Freedom Bible (フリーダム・バイブル)Korean Bible, 1910 (한국어 성경)Bible Mutal (Kosraean)Clementine Vulgate, 1598Baibal Olcim (Matupi Chin)Meriam Mir GospelsOld Persian Version (ترجمه قدیم)Kadede Kap (Pohnpeian New Testament and Psalms)Bíblia Portuguesa Mundial (Brazilian Portuguese)Cornilescu Bible (1924), Cyrillic scriptSynodal Translation (Синодальный перевод)Daničić–Karadžić Bible (1868), CyrillicReina-Valera 1909Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portionsFreedom Bible (Thai)Tongan Bible, Revised West VersionKulish and Puluj Bible (1905)Vietnamese Bible (1923 translation)
vs Chinese Union Vers…

Compare with

Smith–Van Dyck Arabic Bible (فان دايك)Brezhoneg (Breton Gospels, 1827)Judson Burmese Bible (1840)Chamorro: Gospels, Acts and PsalmsChinese Union Version, punctuated (Simplified)Chinese Union Version, punctuated (Traditional)Coptic New TestamentCoptic New Testament (Bohairic)Kralice Bible (1613)Testamenta Marra (Dieri New Testament)Petrus Canisius Bible, 1939 (De Heilige Schrift)Asang Khongca Bible (Eastern Khumi Chin, 2019)Berean Standard BibleDouay-Rheims Bible, American Edition (1899)King James Version with ApocryphaWorld English BibleLondona Biblio (Esperanto, 1910)Louis Segond 1910Lutherbibel 1912Greek New Testament, word by word (STEPBible TAGNT)Greek New Testament: 1904 Patriarchal Text (Byzantine)Greek New Testament: Byzantine Text (Robinson–Pierpont 2018)Greek New Testament: Textus ReceptusSBL Greek New TestamentBaibala Hemolele (Hawaiian Bible, 1868 revision)Modern Hebrew BibleDiodati Bibbia 1885Freedom Bible (フリーダム・バイブル)Korean Bible, 1910 (한국어 성경)Bible Mutal (Kosraean)Clementine Vulgate, 1598Baibal Olcim (Matupi Chin)Meriam Mir GospelsOld Persian Version (ترجمه قدیم)Kadede Kap (Pohnpeian New Testament and Psalms)Bíblia Portuguesa Mundial (Brazilian Portuguese)Cornilescu Bible (1924), Cyrillic scriptSynodal Translation (Синодальный перевод)Daničić–Karadžić Bible (1868), CyrillicReina-Valera 1909Freedom Bible (Thai)Tongan Bible, Revised West VersionKulish and Puluj Bible (1905)Vietnamese Bible (1923 translation)Stop comparing
Aa
Text size
Line width
Verse numbers
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.
1当那一天,耶稣从房子里出来,坐在海边。
2Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
2有许多人到他那里聚集,他只得上船坐下,众人都站在岸上。
3naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
3他用比喻对他们讲许多道理,说:「有一个撒种的出去撒种;
4Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
4撒的时候,有落在路旁的,飞鸟来吃尽了;
5Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
5有落在土浅石头地上的,土既不深,发苗最快,
6Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
6日头出来一晒,因为没有根,就枯干了;
7Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.
7有落在荆棘里的,荆棘长起来,把它挤住了;
8Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.
8又有落在好土里的,就结实,有一百倍的,有六十倍的,有三十倍的。
9Mwenye masikio na asikie!”
9有耳 可听 的,就应当听!」
10Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?”
10门徒进前来,问耶稣说:「对众人讲话,为什么用比喻呢?」
11Yesu akawajibu, “Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
11耶稣回答说:「因为天国的奥秘只叫你们知道,不叫他们知道。
12Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
12凡有的,还要加给他,叫他有余;凡没有的,连他所有的,也要夺去。
13Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
13所以我用比喻对他们讲,是因他们看也看不见,听也听不见,也不明白。
14Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
14在他们身上,正应了 以赛亚 的预言,说: 你们听是要听见,却不明白; 看是要看见,却不晓得;
15Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.
15因为这百姓油蒙了心, 耳朵发沉, 眼睛闭着, 恐怕眼睛看见, 耳朵听见, 心里明白,回转过来, 我就医治他们。
16“Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
16「但你们的眼睛是有福的,因为看见了;你们的耳朵也是有福的,因为听见了。
17Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
17我实在告诉你们,从前有许多先知和义人要看你们所看的,却没有看见,要听你们所听的,却没有听见。」
18“Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
18「所以,你们当听这撒种的比喻。
19Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake.
19凡听见天国道理不明白的,那恶者就来,把所撒在他心里的夺了去;这就是撒在路旁的了。
20Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huo na mara akaupokea kwa furaha.
20撒在石头地上的,就是人听了道,当下欢喜领受,
21Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara.
21只因心里没有根,不过是暂时的,及至为道遭了患难,或是受了逼迫,立刻就跌倒了。
22Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda.
22撒在荆棘里的,就是人听了道,后来有世上的思虑、钱财的迷惑把道挤住了,不能结实。
23Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini.”
23撒在好地上的,就是人听道明白了,后来结实,有一百倍的,有六十倍的,有三十倍的。」
24Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
24耶稣又设个比喻对他们说:「天国好像人撒好种在田里,
25Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake.
25及至人睡觉的时候,有仇敌来,将稗子撒在麦子里就走了。
26Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza kuonekana.
26到长苗吐穗的时候,稗子也显出来。
27Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa magugu yametoka wapi?
27田主的仆人来告诉他说:『主啊,你不是撒好种在田里吗?从哪里来的稗子呢?』
28Yeye akawajibu, Adui ndiye aliyefanya hivyo. Basi, watumishi wake wakamwuliza, Je, unataka twende tukayang'oe
28主人说:『这是仇敌做的。』仆人说:『你要我们去薅出来吗?』
29Naye akawajibu, La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang'oa na ngano pia.
29主人说:『不必,恐怕薅稗子,连麦子也拔出来。
30Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.”
30容这两样一齐长,等着收割。当收割的时候,我要对收割的人说,先将稗子薅出来,捆成捆,留着烧;惟有麦子要收在仓里。』」
31Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake.
31他又设个比喻对他们说:「天国好像一粒芥菜种,有人拿去种在田里。
32Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
32这原是百种里最小的,等到长起来,却比各样的菜都大,且成了树,天上的飞鸟来宿在它的枝上。」
33Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka.”
33他又对他们讲个比喻说:「天国好像面酵,有妇人拿来,藏在三斗面里,直等全团都发起来。」
34Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
34这都是耶稣用比喻对众人说的话;若不用比喻,就不对他们说什么。
35ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
35这是要应验先知的话,说: 我要开口用比喻, 把创世以来所隐藏的事发明出来。
36Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, “Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani.”
36当下,耶稣离开众人,进了房子。他的门徒进前来,说:「请把田间稗子的比喻讲给我们听。」
37Yesu akawaambia, “Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
37他回答说:「那撒好种的就是人子;
38Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.
38田地就是世界;好种就是天国之子;稗子就是那恶者之子;
39Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.
39撒稗子的仇敌就是魔鬼;收割的时候就是世界的末了;收割的人就是天使。
40Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati;
40将稗子薅出来用火焚烧,世界的末了也要如此。
41Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu,
41人子要差遣使者,把一切叫人跌倒的和作恶的,从他国里挑出来,
42na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga meno.
42丢在火炉里;在那里必要哀哭切齿了。
43Kisha, wale wema watang'ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi, kama mna masikio!
43那时,义人在他们父的国里,要发出光来,像太阳一样。有耳 可听 的,就应当听!」
44“Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
44「天国好像宝贝藏在地里,人遇见了就把它藏起来,欢欢喜喜地去变卖一切所有的,买这块地。
45“Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
45天国又好像买卖人寻找好珠子,
46Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile.
46遇见一颗重价的珠子,就去变卖他一切所有的,买了这颗珠子。
47“Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
47天国又好像网撒在海里,聚拢各样水族,
48Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.
48网既满了,人就拉上岸来,坐下,拣好的收在器具里,将不好的丢弃了。
49Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema,
49世界的末了也要这样。天使要出来,从义人中把恶人分别出来,
50na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno.”
50丢在火炉里;在那里必要哀哭切齿了。」
51Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.”
51耶稣说 :「这一切的话你们都明白了吗?」他们说:「我们明白了。」
52Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”
52他说:「凡文士受教作天国的门徒,就像一个家主从他库里拿出新旧的东西来。」
53Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo,
53耶稣说完了这些比喻,就离开那里,
54akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
54来到自己的家乡,在会堂里教训人,甚至他们都希奇,说:「这人从哪里有这等智慧和异能呢?
55Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
55这不是木匠的儿子吗?他母亲不是叫 马利亚 吗?他弟兄们不是叫 雅各 、 约西 、 西门 、 犹大 吗?
56Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?”
56他妹妹们不是都在我们这里吗?这人从哪里有这一切的事呢?」
57Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
57他们就厌弃他。耶稣对他们说:「大凡先知,除了本地本家之外,没有不被人尊敬的。」
58Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.
58耶稣因为他们不信,就在那里不多行异能了。

Tip: use the ← and → keys to turn chapters.