Mathayo 23
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,
1那时,耶稣对众人和门徒讲论,
2“Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose.
2说:「文士和法利赛人坐在 摩西 的位上,
3Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
3凡他们所吩咐你们的,你们都要谨守遵行。但不要效法他们的行为;因为他们能说,不能行。
4Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
4他们把难担的重担捆起来,搁在人的肩上,但自己一个指头也不肯动。
5Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
5他们一切所做的事都是要叫人看见,所以将佩戴的经文做宽了, 衣裳的 子做长了,
6Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi.
6喜爱筵席上的首座,会堂里的高位,
7Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: Mwalimu.
7又喜爱人在街市上问他安,称呼他拉比。
8Lakini ninyi msiitwe kamwe Mwalimu, maana mwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote ni ndugu.
8但你们不要受拉比的称呼,因为只有一位是你们的夫子;你们都是弟兄。
9Wala msimwite mtu yeyote Baba hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni.
9也不要称呼地上的人为父,因为只有一位是你们的父,就是在天上的父。
10Wala msiitwe Viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo.
10也不要受师尊的称呼,因为只有一位是你们的师尊,就是基督。
11Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.
11你们中间谁为大,谁就要作你们的用人。
12Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
12凡自高的,必降为卑;自卑的,必升为高。
13“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie.
13「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们正当人前,把天国 的门 关了,自己不进去,正要进去的人,你们也不容他们进去。
14Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali.
no verse 14 in this text
15“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe.
15「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们走遍洋海陆地,勾引一个人入教,既入了教,却使他作地狱之子,比你们还加倍。
16“Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika.
16「你们这瞎眼领路的有祸了!你们说:『凡指着殿起誓的,这算不得什么;只是凡指着殿中金子起誓的,他就该谨守。』
17Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu?
17你们这无知瞎眼的人哪,什么是大的?是金子呢?还是叫金子成圣的殿呢?
18Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika.
18你们又说:『凡指着坛起誓的,这算不得什么;只是凡指着坛上礼物起誓的,他就该谨守。』
19Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu?
19你们这瞎眼的人哪,什么是大的?是礼物呢?还是叫礼物成圣的坛呢?
20Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake.
20所以,人指着坛起誓,就是指着坛和坛上一切所有的起誓;
21Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake.
21人指着殿起誓,就是指着殿和那住在殿里的起誓;
22Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake.
22人指着天起誓,就是指着 神的宝座和那坐在上面的起誓。
23Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
23「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们将薄荷、茴香、芹菜献上十分之一,那律法上更重的事,就是公义、怜悯、信实,反倒不行了。这 更重的 是你们当行的;那也是不可不行的。
24Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!
24你们这瞎眼领路的,蠓虫你们就滤出来,骆驼你们倒吞下去。
25“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo.
25「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们洗净杯盘的外面,里面却盛满了勒索和放荡。
26Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
26你这瞎眼的法利赛人,先洗净杯盘的里面,好叫外面也干净了。
27“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.
27「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们好像粉饰的坟墓,外面好看,里面却装满了死人的骨头和一切的污秽。
28Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
28你们也是如此,在人前,外面显出公义来,里面却装满了假善和不法的事。
29“Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema.
29「你们这假冒为善的文士和法利赛人有祸了!因为你们建造先知的坟,修饰义人的墓,说:
30Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii!
30『若是我们在我们祖宗的时候,必不和他们同流先知的血。』
31Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua manabii.
31这就是你们自己证明是杀害先知者的子孙了。
32Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza!
32你们去充满你们祖宗的恶贯吧!
33Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?
33你们这些蛇类、毒蛇之种啊,怎能逃脱地狱的刑罚呢?
34Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji.
34所以我差遣先知和智慧人并文士到你们这里来,有的你们要杀害,要钉十字架;有的你们要在会堂里鞭打,从这城追逼到那城,
35Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
35叫世上所流义人的血都归到你们身上,从义人 亚伯 的血起,直到你们在殿和坛中间所杀的 巴拉加 的儿子 撒迦利亚 的血为止。
36Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya.
36我实在告诉你们,这一切的罪都要归到这世代了。」
37“Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
37「 耶路撒冷 啊, 耶路撒冷 啊,你常杀害先知,又用石头打死那奉差遣到你这里来的人。我多次愿意聚集你的儿女,好像母鸡把小鸡聚集在翅膀底下,只是你们不愿意。
38Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.
38看哪,你们的家成为荒场留给你们。
39Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.”
39我告诉你们,从今以后,你们不得再见我,直等到你们说:『奉主名来的是应当称颂的。』」
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.