Mathayo 28
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Baada ya Sabato, karibu na mapambazuko ya siku ile ya Jumapili, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.
1安息日將盡,七日的頭一日,天快亮的時候, 抹大拉 的 馬利亞 和那個 馬利亞 來看墳墓。
2Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
2忽然,地大震動;因為有主的使者從天上下來,把石頭滾開,坐在上面。
3Alionekana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
3他的相貌如同閃電,衣服潔白如雪。
4Walinzi wa lile kaburi wakatetemeka kwa hofu kubwa, hata wakawa kama wamekufa.
4看守的人就因他嚇得渾身亂戰,甚至和死人一樣。
5Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Ninyi msiogope! Najua kwamba mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa.
5天使對婦女說:「不要害怕!我知道你們是尋找那釘十字架的耶穌。
6Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
6他不在這裏,照他所說的,已經復活了。你們來看安放主的地方。
7Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
7快去告訴他的門徒,說他從死裏復活了,並且在你們以先往 加利利 去,在那裏你們要見他。看哪,我已經告訴你們了。」
8Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
8婦女們就急忙離開墳墓,又害怕,又大大地歡喜,跑去要報給他的門徒。
9Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
9忽然,耶穌遇見她們,說:「願你們平安!」她們就上前抱住他的腳拜他。
10Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope! Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, na huko wataniona.”
10耶穌對她們說:「不要害怕!你們去告訴我的弟兄,叫他們往 加利利 去,在那裏必見我。」
11Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
11她們去的時候,看守的兵有幾個進城去,將所經歷的事都報給祭司長。
12Basi, wakakutana pamoja na wazee, na baada ya kushauriana, wakawapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha
12祭司長和長老聚集商議,就拿許多銀錢給兵丁,說:
13wakisema, “Ninyi mtasema hivi: Wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba sisi tukiwa tumelala.
13「你們要這樣說:『夜間我們睡覺的時候,他的門徒來,把他偷去了。』
14Na kama mkuu wa mkoa akijua jambo hili, sisi tutasema naye na kuhakikisha kuwa ninyi hamtapata matatizo.”
14倘若這話被巡撫聽見,有我們勸他,保你們無事。」
15Wale walinzi wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Habari hiyo imeenea kati ya Wayahudi mpaka leo.
15兵丁受了銀錢,就照所囑咐他們的去行。這話就傳說在 猶太 人中間,直到今日。
16Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.
16十一個門徒往 加利利 去,到了耶穌約定的山上。
17Walipomwona, wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka.
17他們見了耶穌就拜他,然而還有人疑惑。
18Yesu akaja karibu, akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
18耶穌進前來,對他們說:「天上地下所有的權柄都賜給我了。
19Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
19所以,你們要去,使萬民作我的門徒,奉父、子、聖靈的名給他們施洗 。
20Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati.”
20凡我所吩咐你們的,都教訓他們遵守,我就常與你們同在,直到世界的末了。」
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.