Waebrania 1
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,
1上帝既在古時藉着眾先知多次多方地曉諭列祖,
2lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu na akamteua avimiliki vitu vyote.
2就在這末世藉着他兒子曉諭我們;又早已立他為承受萬有的,也曾藉着他創造諸世界。
3Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
3他是上帝榮耀所發的光輝,是上帝本體的真像,常用他權能的命令托住萬有。他洗淨了人的罪,就坐在高天至大者的右邊。
4Mwana ni mkuu zaidi kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu zaidi kuliko jina lao.
4他所承受的名,既比天使的名更尊貴,就遠超過天使。
5Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; Mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.”
5所有的天使,上帝從來對哪一個說: 你是我的兒子, 我今日生你? 又指着哪一個說: 我要作他的父, 他要作我的子?
6Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, alisema: “Malaika wote wa Mungu wanapaswa kumwabudu.”
6再者,上帝使長子到世上來的時候,就說: 上帝的使者都要拜他。
7Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema: “Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa ndimi za moto.”
7論到使者,又說: 上帝以風為使者, 以火焰為僕役;
8Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema: “Utawala wako ee Mungu, wadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
8論到子卻說: 上帝啊,你的寶座是永永遠遠的; 你的國權是正直的。
9Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa zaidi kuliko wenzako.”
9你喜愛公義,恨惡罪惡; 所以上帝,就是你的上帝,用喜樂油膏你, 勝過膏你的同伴;
10Pia alisema: “Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako.
10又說:主啊,你起初立了地的根基; 天也是你手所造的。
11Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi.
11天地都要滅沒,你卻要長存。 天地都要像衣服漸漸舊了;
12Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
12你要將天地捲起來,像一件外衣, 天地就都改變了。 惟有你永不改變; 你的年數沒有窮盡。
13Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.”
13所有的天使,上帝從來對哪一個說: 你坐在我的右邊, 等我使你仇敵作你的腳凳?
14Malaika ni roho tu wanaomtumikia Mungu, na Mungu huwatuma wawasaidie wale watakaopokea wokovu.
14天使豈不都是服役的靈、奉差遣為那將要承受救恩的人效力嗎?
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.