Waebrania 3
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
1同蒙天召的聖潔弟兄啊,你們應當思想我們所認為使者、為大祭司的耶穌。
2Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
2他為那設立他的盡忠,如同 摩西 在上帝的全家盡忠一樣。
3Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalika naye Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
3他比 摩西 算是更配多得榮耀,好像建造房屋的比房屋更尊榮;
4Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani—na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
4因為房屋都必有人建造,但建造萬物的就是上帝。
5Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
5摩西 為僕人,在上帝的全家誠然盡忠,為要證明將來必傳說的事。
6Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile tunachotumainia.
6但基督為兒子,治理上帝的家;我們若將可誇的盼望和膽量堅持到底,便是他的家了。
7Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
7聖靈有話說: 你們今日若聽他的話,
8msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu; kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,
8就不可硬着心, 像在曠野惹他發怒、 試探他的時候一樣。
9Huko wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, asema Bwana, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu kwa miaka arobaini.
9在那裏,你們的祖宗試我探我, 並且觀看我的作為有四十年之久。
10Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.
10所以,我厭煩那世代的人,說: 他們心裏常常迷糊, 竟不曉得我的作為!
11Basi, nilikasirika, nikaapa: Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko.”
11我就在怒中起誓說: 他們斷不可進入我的安息。
12Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
12弟兄們,你們要謹慎,免得你們中間或有人存着不信的惡心,把永生上帝離棄了。
13Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
13總要趁着還有今日,天天彼此相勸,免得你們中間有人被罪迷惑,心裏就剛硬了。
14Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
14我們若將起初確實的信心堅持到底,就在基督裏有分了。
15Maandiko yasema hivi: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu.”
15經上 說:「你們今日若聽他的話,就不可硬着心,像惹他發怒的日子一樣。」
16Ni akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
16那時,聽見他話惹他發怒的是誰呢?豈不是跟着 摩西 從 埃及 出來的眾人嗎?
17Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
17上帝四十年之久,又厭煩誰呢?豈不是那些犯罪、屍首倒在曠野的人嗎?
18Mungu alipoapa: “Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
18又向誰起誓,不容他們進入他的安息呢?豈不是向那些不信從的人嗎?
19Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
19這樣看來,他們不能進入 安息 是因為不信的緣故了。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.