Warumi 12
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
1所以,弟兄們,我以上帝的慈悲勸你們,將身體獻上,當作活祭,是聖潔的,是上帝所喜悅的;你們如此事奉乃是理所當然的。
2Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
2不要效法這個世界,只要心意更新而變化,叫你們察驗何為上帝的善良、純全、可喜悅的旨意。
3Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
3我憑着所賜我的恩對你們各人說:不要看自己過於所當看的;要照着上帝所分給各人信心的大小,看得合乎中道。
4Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
4正如我們一個身子上有好些肢體,肢體也不都是一樣的用處。
5Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
5我們這許多人,在基督裏成為一身,互相聯絡作肢體,也是如此。
6Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
6按我們所得的恩賜,各有不同。或說預言,就當照着信心的程度說 預言 ;
7Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
7或作執事,就當 專一 執事;或作教導的,就當 專一 教導;
8Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
8或作勸化的,就當 專一 勸化;施捨的,就當誠實;治理的,就當殷勤;憐憫人的,就當甘心。
9Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
9愛人不可虛假。惡,要厭惡;善,要親近。
10Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
10愛弟兄,要彼此親熱;恭敬人,要彼此推讓。
11Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
11殷勤,不可懶惰;要心裏火熱,常常服事主。
12Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
12在指望中要喜樂;在患難中要忍耐;禱告要恆切。
13Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
13聖徒缺乏,要幫補;客,要一味地款待。
14Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.
14逼迫你們的,要給他們祝福;只要祝福,不可咒詛。
15Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
15與喜樂的人要同樂;與哀哭的人要同哭。
16Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.
16要彼此同心;不要志氣高大,倒要俯就卑微的人。不要自以為聰明。
17Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.
17不要以惡報惡;眾人以為美的事要留心去做。
18Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.
18若是能行,總要盡力與眾人和睦。
19Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana.”
19親愛的弟兄,不要自己伸冤,寧可讓步,聽憑主怒;因為 經上 記着:「主說:『伸冤在我,我必報應。』」
20Tena, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
20所以,「你的仇敵若餓了,就給他吃,若渴了,就給他喝;因為你這樣行就是把炭火堆在他的頭上。」
21Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
21你不可為惡所勝,反要以善勝惡。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.