馬太福音 27
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1到了早晨,眾祭司長和民間的長老大家商議要治死耶穌,
1Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
2就把他捆綁,解去,交給巡撫 彼拉多 。
2Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.
3這時候,賣耶穌的 猶大 看見耶穌已經定了罪,就後悔,把那三十塊錢拿回來給祭司長和長老,說:
3Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha.
4「我賣了無辜之人的血是有罪了。」他們說:「那與我們有甚麼相干?你自己承當吧!」
4Akawaambia, “Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe.” Lakini wao wakasema, “Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako.”
5猶大 就把那銀錢丟在殿裏,出去吊死了。
5Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.
6祭司長拾起銀錢來,說:「這是血價,不可放在庫裏。」
6Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
7他們商議,就用那銀錢買了窯戶的一塊田,為要埋葬外鄉人。
7Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
8所以那塊田直到今日還叫做「血田」。
8Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
9這就應了先知 耶利米 的話,說:「他們用那三十塊錢,就是被估定之人的價錢,是 以色列 人中所估定的,
9Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,
10買了窯戶的一塊田;這是照着主所吩咐我的。」
10wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.”
11耶穌站在巡撫面前;巡撫問他說:「你是 猶太 人的王嗎?」耶穌說:「你說的是。」
11Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, “Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamwambia, “Wewe umesema.”
12他被祭司長和長老控告的時候,甚麼都不回答。
12Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
13彼拉多 就對他說:「他們作見證告你這麼多的事,你沒有聽見嗎?」
13Hivyo Pilato akamwuliza, “Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?”
14耶穌仍不回答,連一句話也不說,以致巡撫甚覺希奇。
14Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.
15巡撫有一個常例,每逢這節期,隨眾人所要的釋放一個囚犯給他們。
15Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
16當時有一個出名的囚犯叫 巴拉巴 。
16Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
17眾人聚集的時候, 彼拉多 就對他們說:「你們要我釋放哪一個給你們?是 巴拉巴 呢?是稱為基督的耶穌呢?」
17Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, “Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba ama Yesu aitwae Kristo?”
18巡撫原知道他們是因為嫉妒才把他解了來。
18Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.
19正坐堂的時候,他的夫人打發人來說:「這義人的事,你一點不可管,因為我今天在夢中為他受了許多的苦。」
19Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: “Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”
20祭司長和長老挑唆眾人,求釋放 巴拉巴 ,除滅耶穌。
20Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.
21巡撫對眾人說:「這兩個人,你們要我釋放哪一個給你們呢?」他們說:「 巴拉巴 。」
21Mkuu wa mkoa akawauliza, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?” Wakamjibu, “Baraba!”
22彼拉多 說:「這樣,那稱為基督的耶穌我怎麼辦他呢?」他們都說:「把他釘十字架!」
22Pilato akawauliza, “Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?” Wote wakasema, “Asulubiwe!”
23巡撫說:「為甚麼呢?他做了甚麼惡事呢?」他們便極力地喊着說:「把他釘十字架!」
23Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Wao wakazidi kupaaza sauti: “Asulubiwe!”
24彼拉多 見說也無濟於事,反要生亂,就拿水在眾人面前洗手,說:「流這義人的血,罪不在我,你們承當吧。」
24Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”
25眾人都回答說:「他的血歸到我們和我們的子孫身上。」
25Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
26於是 彼拉多 釋放 巴拉巴 給他們,把耶穌鞭打了,交給人釘十字架。
26Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.
27巡撫的兵就把耶穌帶進衙門,叫全營的兵都聚集在他那裏。
27Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.
28他們給他脫了衣服,穿上一件朱紅色袍子,
28Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
29用荊棘編做冠冕,戴在他頭上,拿一根葦子放在他右手裏,跪在他面前,戲弄他,說:「恭喜, 猶太 人的王啊!」
29Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, “Shikamoo mfalme wa Wayahudi!”
30又吐唾沫在他臉上,拿葦子打他的頭。
30Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
31戲弄完了,就給他脫了袍子,仍穿上他自己的衣服,帶他出去,要釘十字架。
31Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
32他們出來的時候,遇見一個 古利奈 人,名叫 西門 ,就勉強他同去,好背着耶穌的十字架。
32Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
33到了一個地方名叫 各各他 ,意思就是「髑髏地」。
33Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu la kichwa,”
34兵丁拿苦膽調和的酒給耶穌喝;他嘗了,就不肯喝。
34wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
35他們既將他釘在十字架上,就拈鬮分他的衣服,
35Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
36又坐在那裏看守他。
36Wakaketi, wakawa wanamchunga.
37在他頭以上安一個牌子,寫着他的罪狀,說:「這是 猶太 人的王耶穌。」
37Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, “Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi.”
38當時,有兩個強盜和他同釘十字架,一個在右邊,一個在左邊。
38Wanyang'anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
39從那裏經過的人譏誚他,搖着頭,說:
39Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,
40「你這拆毀 聖 殿、三日又建造起來的,可以救自己吧!你如果是上帝的兒子,就從十字架上下來吧!」
40“Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!”
41祭司長和文士並長老也是這樣戲弄他,說:
41Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,
42「他救了別人,不能救自己。他是 以色列 的王,現在可以從十字架上下來,我們就信他。
42“Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
43他倚靠上帝,上帝若喜悅他,現在可以救他;因為他曾說:『我是上帝的兒子。』」
43Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka.”
44那和他同釘的強盜也是這樣地譏誚他。
44Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
45從午正到申初,遍地都黑暗了。
45Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
46約在申初,耶穌大聲喊着說:「以利!以利!拉馬撒巴各大尼?」就是說:「我的上帝!我的上帝!為甚麼離棄我?」
46Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eli, Eli, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
47站在那裏的人,有的聽見就說:「這個人呼叫 以利亞 呢!」
47Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, “Anamwita Eliya.”
48內中有一個人趕緊跑去,拿海絨蘸滿了醋,綁在葦子上,送給他喝。
48Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
49其餘的人說:「且等着,看 以利亞 來救他不來。」
49Wengine wakasema, “Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.”
50耶穌又大聲喊叫,氣就斷了。
50Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.
51忽然,殿裏的幔子從上到下裂為兩半,地也震動,磐石也崩裂,
51Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52墳墓也開了,已睡聖徒的身體多有起來的。
52makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;
53到耶穌復活以後,他們從墳墓裏出來,進了聖城,向許多人顯現。
53nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.
54百夫長和一同看守耶穌的人看見地震並所經歷的事,就極其害怕,說:「這真是上帝的兒子了!」
54Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
55有好些婦女在那裏,遠遠地觀看;她們是從 加利利 跟隨耶穌來服事他的。
55Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
56內中有 抹大拉 的 馬利亞 ,又有 雅各 和 約西 的母親 馬利亞 ,並有 西庇太 兩個兒子的母親。
56Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
57到了晚上,有一個財主,名叫 約瑟 ,是 亞利馬太 來的,他也是耶穌的門徒。
57Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
58這人去見 彼拉多 ,求耶穌的身體; 彼拉多 就吩咐給他。
58Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.
59約瑟 取了身體,用乾淨細麻布裹好,
59Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
60安放在自己的新墳墓裏,就是他鑿在磐石裏的。他又把大石頭滾到墓門口,就去了。
60akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
61有 抹大拉 的 馬利亞 和那個 馬利亞 在那裏,對着墳墓坐着。
61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.
62次日,就是預備日的第二天,祭司長和法利賽人聚集來見 彼拉多 ,說:
62Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
63「大人,我們記得那誘惑人的還活着的時候曾說:『三日後我要復活。』
63Wakasema, “Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baada ya siku tatu nitafufuka.
64因此,請吩咐人將墳墓把守妥當,直到第三日,恐怕他的門徒來,把他偷了去,就告訴百姓說:『他從死裏復活了。』這樣,那後來的迷惑比先前的更利害了!」
64Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali.”
65彼拉多 說:「你們有看守的兵,去吧!盡你們所能的把守妥當。」
65Pilato akawaambia, “Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo.”
66他們就帶着看守的兵同去,封了石頭,將墳墓把守妥當。
66Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.