Marko 14
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
1过两天是逾越 节 ,又是除酵节,祭司长和文士想法子怎么用诡计捉拿耶稣,杀他。
2Lakini walisema, “Tusimtie nguvuni wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
2只是说:「当节的日子不可,恐怕百姓生乱。」
3Yesu alikuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, Mkoma. Alipokuwa mezani kula chakula, mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya nardo safi ya thamani kubwa alikuja, akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu marashi hayo kichwani.
3耶稣在 伯大尼 长大麻风的 西门 家里坐席的时候,有一个女人拿着一玉瓶至贵的真哪哒香膏来,打破玉瓶,把膏浇在耶稣的头上。
4Baadhi ya watu waliokuwa hapo walikasirika wakajisemea, “Kwa nini kupoteza ovyo marashi haya?
4有几个人心中很不喜悦,说:「何用这样枉费香膏呢?
5Yangaliweza kuuzwa kwa fedha kiasi cha denari mia tatu, wakapewa maskini!” Wakamkemea huyo mama.
5这香膏可以卖三十多两银子周济穷人。」他们就向那女人生气。
6Lakini Yesu akawaambia, “Mwacheni; kwa nini mnamsumbua? Amenitendea jambo jema.
6耶稣说:「由她吧!为什么难为她呢?她在我身上做的是一件美事。
7Maskini mnao daima pamoja nanyi; mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
7因为常有穷人和你们同在,要向他们行善随时都可以;只是你们不常有我。
8Yeye amefanya alivyoweza; ameupaka mwili wangu marashi kuutayarisha kwa maziko.
8她所做的,是尽她所能的;她是为我安葬的事把香膏预先浇在我身上。
9Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni Habari Njema itakapohubiriwa, kitendo hiki alichofanya kitatajwa kwa ajili ya kumkumbuka.”
9我实在告诉你们,普天之下,无论在什么地方传这福音,也要述说这女人所做的,以为记念。」
10Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, alienda kwa makuhani wakuu ili kumsaliti Yesu.
10十二门徒之中,有一个 加略 人 犹大 去见祭司长,要把耶稣交给他们。
11Makuhani wakuu waliposikia habari hiyo, walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Basi, Yuda akaanza kutafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.
11他们听见就欢喜,又应许给他银子;他就寻思如何得便把耶稣交给他们。
12Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza, “Wataka tukuandalie wapi karamu ya Pasaka?”
12除酵节的第一天,就是宰逾越 羊羔 的那一天,门徒对耶稣说:「你吃逾越 节的筵席 要我们往哪里去预备呢?」
13Basi Yesu akawatuma wawili wa wanafunzi wake akiwaambia, “Nendeni mjini, nanyi mtakutana na mtu anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni
13耶稣就打发两个门徒,对他们说:「你们进城去,必有人拿着一瓶水迎面而来,你们就跟着他。
14mpaka katika nyumba atakayoingia, mkamwambie mwenye nyumba, Mwalimu anasema: wapi chumba changu ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?
14他进哪家去,你们就对那家的主人说:『夫子说:客房在哪里?我与门徒好在那里吃逾越 节的筵席 。』
15Naye atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichotayarishwa na kupambwa. Tuandalieni humo.”
15他必指给你们摆设整齐的一间大楼,你们就在那里为我们预备。」
16Wanafunzi wakaondoka, wakaenda mjini, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Wakaandaa karamu ya Pasaka.
16门徒出去,进了城,所遇见的正如耶稣所说的。他们就预备了逾越 节的筵席 。
17Ilipokuwa jioni, Yesu alifika pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
17到了晚上,耶稣和十二个门徒都来了。
18Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.”
18他们坐席正吃的时候,耶稣说:「我实在告诉你们,你们中间有一个与我同吃的人要卖我了。」
19Hapo wanafunzi wake wakaanza kuhuzunika, wakamwuliza mmojammoja, “Je, ni mimi?”
19他们就忧愁起来,一个一个地问他说:「是我吗?」
20Yesu akawaambia, “Ni mmoja wenu ninyi kumi na wawili, anayechovya mkate pamoja nami katika bakuli.
20耶稣对他们说:「是十二个门徒中同我蘸手在盘子里的那个人。
21Kweli Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yanavyosema juu yake; lakini, ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa!”
21人子必要去世,正如 经上 指着他所写的;但卖人子的人有祸了!那人不生在世上倒好。」
22Walipokuwa wanakula, Yesu alitwaa mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni; huu ni mwili wangu.”
22他们吃的时候,耶稣拿起饼来,祝了福,就擘开,递给他们,说:「你们拿着吃,这是我的身体」;
23Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa; nao wote wakanywa katika kikombe hicho.
23又拿起杯来,祝谢了,递给他们;他们都喝了。
24Akawaambia, “Hii ni damu yangu inayothibitisha agano la Mungu, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi.
24耶稣说:「这是我立约的血,为多人流出来的。
25Kweli nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa upya katika Ufalme wa Mungu.”
25我实在告诉你们,我不再喝这葡萄汁,直到我在 神的国里喝新的那日子。」
26Kisha wakaimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
26他们唱了诗,就出来,往 橄榄山 去。
27Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami; maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampiga mchungaji nao kondoo watatawanyika.
27耶稣对他们说:「你们都要跌倒了,因为 经上 记着说: 我要击打牧人, 羊就分散了。
28Lakini nikisha fufuka, nitawatangulieni kule Galilaya.”
28但我复活以后,要在你们以先往 加利利 去。」
29Petro akamwambia “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakukana kamwe!”
29彼得 说:「众人虽然跌倒,我总不能。」
30Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.”
30耶稣对他说:「我实在告诉你,就在今天夜里,鸡叫两遍以先,你要三次不认我。」
31Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakuacha kamwe.” Wanafunzi wote pia wakasema vivyo hivyo.
31彼得 却极力地说:「我就是必须和你同死,也总不能不认你。」众门徒都是这样说。
32Basi, wakafika katika bustani iitwayo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati mimi nasali.”
32他们来到一个地方,名叫 客西马尼 。耶稣对门徒说:「你们坐在这里,等我祷告。」
33Kisha akawachukua Petro, Yakobo na Yohane; akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.
33于是带着 彼得 、 雅各 、 约翰 同去,就惊恐起来,极其难过,
34Akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe.”
34对他们说:「我心里甚是忧伤,几乎要死;你们在这里等候,警醒。」
35Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi, akasali kwamba, kama ingewezekana, asiipitie saa hiyo ya mateso.
35他就稍往前走,俯伏在地,祷告说:「倘若可行,便叫那时候过去。」
36Akasema, “Baba yangu, kwako mambo yote yanawezekana. Uniondolee kikombe hiki; lakini isiwe kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”
36他说:「阿爸!父啊!在你凡事都能;求你将这杯撤去。然而,不要从我的意思,只要从你的意思。」
37Kisha akarudi kwa wanafunzi wale watatu, akawakuta wamelala. Basi, akamwuliza Petro, “Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?”
37耶稣回来,见他们睡着了,就对 彼得 说:「 西门 ,你睡觉吗?不能警醒片时吗?
38Kisha akawaambia, “Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
38总要警醒祷告,免得入了迷惑。你们心灵固然愿意,肉体却软弱了。」
39Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale.
39耶稣又去祷告,说的话还是与先前一样,
40Kisha akarudi tena, akawakuta wamelala. Macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Hawakujua la kumjibu.
40又来见他们睡着了,因为他们的眼睛甚是困倦;他们也不知道怎么回答。
41Alipowajia mara ya tatu aliwaambia, “Mnalala bado na kupumzika? Sasa imetosha! Saa imefika! Mwana wa Mtu anakabidhiwa kwa watu waovu.
41第三次来,对他们说:「现在你们仍然睡觉安歇吧!够了,时候到了。看哪,人子被卖在罪人手里了。
42Amkeni, twendeni zetu. Tazameni, yule atakayenisaliti amekaribia.”
42起来!我们走吧。看哪,那卖我的人近了!」
43Yesu alipokuwa bado anasema, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee.
43说话之间,忽然那十二个门徒里的 犹大 来了,并有许多人带着刀棒,从祭司长和文士并长老那里与他同来。
44Msaliti Yuda alikuwa amewapa ishara: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni, mkampeleke chini ya ulinzi.”
44卖耶稣的人曾给他们一个暗号,说:「我与谁亲嘴,谁就是他。你们把他拿住,牢牢靠靠地带去。」
45Yuda alipofika tu, alimwendea Yesu moja kwa moja, akasema, “Mwalimu!” Kisha akambusu.
45犹大 来了,随即到耶稣跟前,说:「拉比」,便与他亲嘴。
46Basi, hao watu wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
46他们就下手拿住他。
47Mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja na Yesu akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
47旁边站着的人,有一个拔出刀来,将大祭司的仆人砍了一刀,削掉了他一个耳朵。
48Yesu akawaambia, “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?
48耶稣对他们说:「你们带着刀棒出来拿我,如同拿强盗吗?
49Kila siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini sasa lazima Maandiko Matakatifu yatimie.”
49我天天教训人,同你们在殿里,你们并没有拿我。但 这事成就 ,为要应验经上的话。」
50Hapo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
50门徒都离开他,逃走了。
51Kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anamfuata Yesu akiwa amevaa shuka. Nao wakajaribu kumkamata.
51有一个少年人,赤身披着一块麻布,跟随耶稣,众人就捉拿他。
52Lakini yeye akaponyoka, akaiachilia ile shuka, akakimbia uchi.
52他却丢了麻布,赤身逃走了。
53Basi, wakampeleka Yesu kwa Kuhani Mkuu ambapo makuhani wakuu wote, wazee na walimu wa Sheria walikuwa wamekutanika.
53他们把耶稣带到大祭司那里,又有众祭司长和长老并文士都来和大祭司一同聚集。
54Petro alimfuata Yesu kwa mbali, akaingia ndani ya ya wa Kuhani Mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto.
54彼得 远远地跟着耶稣,一直进入大祭司的院里,和差役一同坐在火光里烤火。
55Makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu wapate kumwua, lakini hawakupata.
55祭司长和全公会寻找见证控告耶稣,要治死他,却寻不着。
56Watu wengi walitoa ushahidi wa uongo juu ya Yesu, lakini ushahidi wao haukupatana.
56因为有好些人作假见证告他,只是他们的见证各不相合。
57Kisha wengine walisimama, wakatoa ushahidi wa uongo wakisema:
57又有几个人站起来作假见证告他,说:
58“Tulimsikia mtu huyu akisema, Nitaliharibu Hekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono.”
58「我们听见他说:『我要拆毁这人手所造的殿,三日内就另造一座不是人手所造的。』」
59Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukupatana.
59他们就是这么作见证,也是各不相合。
60Basi, Kuhani Mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
60大祭司起来站在中间,问耶稣说:「你什么都不回答吗?这些人作见证告你的是什么呢?」
61Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”
61耶稣却不言语,一句也不回答。大祭司又问他说:「你是那当称颂者的儿子基督不是?」
62Yesu akajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa Mwenyezi, akija katika mawingu ya mbinguni.”
62耶稣说:「我是。你们必看见人子坐在那权能者的右边,驾着天上的云降临。」
63Hapo Kuhani Mkuu akararua joho lake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi?
63大祭司就撕开衣服,说:「我们何必再用见证人呢?
64Mmesikia kufuru yake! Ninyi mwaonaje?” Wote wakaamua kwamba anastahili kuuawa.
64你们已经听见他这僭妄的话了。你们的意见如何?」他们都定他该死的罪。
65Basi, baadhi yao wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, wakampiga na kumwambia, “Bashiri ni nani aliyekupiga!” Hata watumishi wakamchukua, wakampiga makofi.
65就有人吐唾沫在他脸上,又蒙着他的脸,用拳头打他,对他说:「你说预言吧!」差役接过他来,用手掌打他。
66Petro alipokuwa bado chini ukumbini, mmoja wa wajakazi wa kuhani Mkuu alikuja.
66彼得 在下边院子里;来了大祭司的一个使女,
67Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama, akamwambia, “Hata wewe ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”
67见 彼得 烤火,就看着他,说:「你素来也是同 拿撒勒 人耶稣一伙的。」
68Lakini Petro akakana, “Sijui, wala sielewi unayosema!” Kisha Petro akaondoka, akaenda nje uani. Hapo jogoo akawika.
68彼得 却不承认,说:「我不知道,也不明白你说的是什么。」于是出来,到了前院,鸡就叫了。
69Yule mjakazi alipomwona tena Petro, akaanza tena kuwaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, “Mtu huyu ni mmoja wao.”
69那使女看见他,又对旁边站着的人说:「这也是他们一党的。」
70Petro akakana tena. Baadaye kidogo, watu waliokuwa wamesimama hapo wakamwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, maana wewe ni Mgalilaya.”
70彼得 又不承认。过了不多的时候,旁边站着的人又对 彼得 说:「你真是他们一党的!因为你是 加利利 人。」
71Lakini Petro akaanza kulaani na kuapa akisema, “Mimi simjui mtu huyu mnayesema habari zake.”
71彼得 就发咒起誓地说:「我不认得你们说的这个人。」
72Hapo jogoo akawika mara ya pili. Basi, Petro akakumbuka jinsi Yesu alivyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Petro akabubujika machozi.
72立时鸡叫了第二遍。 彼得 想起耶稣对他所说的话:「鸡叫两遍以先,你要三次不认我。」思想起来,就哭了。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.