Marko 2
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani.
1过了些日子,耶稣又进了 迦百农 。人听见他在房子里,
2Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,
2就有许多人聚集,甚至连门前都没有空地;耶稣就对他们讲道。
3wakati mtu mmoja aliyepooza alipoletwa kwake akiwa amechukuliwa na watu wanne.
3有人带着一个瘫子来见耶稣,是用四个人抬来的;
4Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya dari iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
4因为人多,不得近前,就把耶稣所在的房子,拆了房顶,既拆通了,就把瘫子连所躺卧的褥子都缒下来。
5Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.”
5耶稣见他们的信心,就对瘫子说:「小子,你的罪赦了。」
6Baadhi ya walimu wa Sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao,
6有几个文士坐在那里,心里议论,说:
7“Anathubutuje kusema hivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake.”
7「这个人为什么这样说呢?他说僭妄的话了。除了 神以外,谁能赦罪呢?」
8Yesu alitambua mara mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu?
8耶稣心中知道他们心里这样议论,就说:「你们心里为什么这样议论呢?
9Ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, Umesamehewa dhambi zako, au kumwambia, Inuka! Chukua mkeka wako utembee?
9或对瘫子说『你的罪赦了』,或说『起来!拿你的褥子行走』,哪一样容易呢?
10Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza,
10但要叫你们知道,人子在地上有赦罪的权柄。」就对瘫子说:
11“Nakwambia simama, chukua mkeka wako uende nyumbani!”
11「我吩咐你,起来!拿你的褥子回家去吧。」
12Mara, watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka, akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wote wakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, “Hatujapata kamwe kuona jambo kama hili.”
12那人就起来,立刻拿着褥子,当众人面前出去了,以致众人都惊奇,归荣耀与 神,说:「我们从来没有见过这样的事!」
13Yesu alikwenda tena kando ya ziwa. Umati wa watu ukamwendea, naye akaanza kuwafundisha.
13耶稣又出到海边去,众人都就了他来,他便教训他们。
14Alipokuwa akipita, akamwona Lawi mwana wa Alfayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Lawi akasimama, akamfuata.
14耶稣经过的时候,看见 亚勒腓 的儿子 利未 坐在税关上,就对他说:「你跟从我来。」他就起来,跟从了耶稣。
15Baadaye, Yesu alikuwa amekaa mezani, nyumbani kwa Lawi, kula chakula. Watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuwa wamemfuata Yesu na wengi wao wakawa wamekaa mezani pamoja naye na wanafunzi wake.
15耶稣在 利未 家里坐席的时候,有好些税吏和罪人与耶稣并门徒一同坐席;因为这样的人多,他们也跟随耶稣。
16Basi, baadhi ya walimu wa Sheria ambao walikuwa Mafarisayo walipomwona Yesu akila pamoja na watu wenye dhambi na watoza ushuru, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”
16法利赛人中的文士看见耶稣和罪人并税吏一同吃饭,就对他门徒说:「他和税吏并罪人一同吃喝吗?」
17Yesu alipowasikia, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.”
17耶稣听见,就对他们说:「康健的人用不着医生,有病的人才用得着。我来本不是召义人,乃是召罪人。」
18Wakati mmoja wanafunzi wa Yohane na wanafunzi wa Mafarisayo walikuwa wanafunga. Basi, watu wakaja, wakamwuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wa Yohane na wa Mafarisayo wanafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
18当下, 约翰 的门徒和法利赛人禁食。他们来问耶稣说:「 约翰 的门徒和法利赛人的门徒禁食,你的门徒倒不禁食,这是为什么呢?」
19Yesu akajibu, “Walioalikwa harusini wanawezaje kufunga kama bwana harusi yupo pamoja nao? Wakati wote wawapo pamoja na bwana harusi hawawezi kufunga.
19耶稣对他们说:「新郎和陪伴之人同在的时候,陪伴之人岂能禁食呢?新郎还同在,他们不能禁食。
20Lakini wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
20但日子将到,新郎要离开他们,那日他们就要禁食。
21“Hakuna mtu anayekata kiraka kutoka katika nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama akifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
21没有人把新布缝在旧衣服上,恐怕所补上的新布带坏了旧衣服,破的就更大了。
22Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai itavipasua hivyo viriba, nayo divai pamoja na hivyo viriba vitaharibika. Divai mpya hutiwa katika viriba vipya!”
22也没有人把新酒装在旧皮袋里,恐怕酒把皮袋裂开,酒和皮袋就都坏了;惟把新酒装在新皮袋里。」
23Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano.
23耶稣当安息日从麦地经过。他门徒行路的时候,掐了麦穗。
24Mafarisayo wakawaambia, “Tazama! Kwa nini wanafanya jambo ambalo si halali kufanya wakati wa Sabato?”
24法利赛人对耶稣说:「看哪,他们在安息日为什么做不可做的事呢?」
25Yesu akawajibu, “Je, hamjapata kusoma juu ya kile alichofanya Daudi wakati alipohitaji chakula? Yeye pamoja na wenzake waliona njaa,
25耶稣对他们说:「 经上记着 大卫 和跟从他的人缺乏饥饿之时所做的事,你们没有念过吗?
26naye akaingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa Kuhani Mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”
26他当 亚比亚他 作大祭司的时候,怎么进了 神的殿,吃了陈设饼,又给跟从他的人吃。这饼除了祭司以外,人都不可吃。」
27Basi, Yesu akawaambia, “Sabato iliwekwa kwa ajili ya binadamu na si binadamu kwa ajili ya Sabato!
27又对他们说:「安息日是为人设立的,人不是为安息日设立的。
28Kwa hiyo, Mwana wa Mtu ni Bwana hata wa Sabato.”
28所以,人子也是安息日的主。」
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.