Waebrania 10
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Sheria ya Wayahudi si picha kamili ya mambo yale halisi: ni kivuli tu cha mema yanayokuja. Dhabihu zilezile hutolewa daima, mwaka baada ya mwaka. Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihu hizo, kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu?
1律法既是将来美事的影儿,不是本物的真像,总不能借着每年常献一样的祭物叫那近前来的人得以完全。
2Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na dhabihu hizo zote zingekoma.
2若不然,献祭的事岂不早已止住了吗?因为礼拜的人,良心既被洁净,就不再觉得有罪了。
3Lakini dhabihu hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao.
3但这些 祭物 是叫人每年想起罪来;
4Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
4因为公牛和山羊的血,断不能除罪。
5Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu: “Hukutaka dhabihu wala sadaka, lakini umenitayarishia mwili.
5所以基督到世上来的时候,就说: 神啊 ,祭物和礼物是你不愿意的; 你曾给我预备了身体。
6Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.
6燔祭和赎罪 祭 是你不喜欢的。
7Hapo nikasema: Niko hapa ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha Sheria.”
7那时我说: 神啊,我来了, 为要照你的旨意行; 我的事在经卷上已经记载了。
8Kwanza alisema: “Hutaki, wala hupendezwi na dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na Sheria.
8以上说:「祭物和礼物,燔祭和赎罪祭,是你不愿意的,也是你不喜欢的(这都是按着律法献的)」;
9Kisha akasema: “Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako.” Hivyo Mungu alibatilisha dhabihu za zamani na mahali pake akaweka dhabihu nyingine moja.
9后又说:「我来了为要照你的旨意行」; 可见 他是除去在先的,为要立定在后的。
10Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza mapenzi ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile dhabihu ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha.
10我们凭这旨意,靠耶稣基督,只一次献上他的身体,就得以成圣。
11Kila kuhani Myahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoa dhabibu zilezile mara nyingi, dhabibu ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
11凡祭司天天站着事奉 神 ,屡次献上一样的祭物,这祭物永不能除罪。
12Lakini Kristo alitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi, dhabihu ifaayo milele, kisha akaketi upande wa kulia wa Mungu.
12但基督献了一次永远的赎罪祭,就在 神的右边坐下了。
13Huko anangoja mpaka adui zake watakapowekwa kama kibao chini ya miguu yake.
13从此,等候他仇敌成了他的脚凳。
14Basi, kwa dhabihu yake moja tu, amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wanaotakaswa dhambi zao.
14因为他一次献祭,便叫那得以成圣的人永远完全。
15Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:
15圣灵也对我们作见证;因为他既已说过:
16“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, katika siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
16主说:那些日子以后, 我与他们所立的约乃是这样: 我要将我的律法写在他们心上, 又要放在他们的里面。
17Kisha akaongeza kusema: “Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendo vyao vya uhalifu.”
17以后就说 : 我不再记念他们的罪愆和他们的过犯。
18Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa dhabihu za kuondoa dhambi.
18这些罪过既已赦免,就不用再为罪献祭了。
19Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu.
19弟兄们,我们既因耶稣的血得以坦然进入至圣所,
20Yeye ametufungulia njia mpya na yenye uzima kupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wake mwenyewe.
20是借着他给我们开了一条又新又活的路,从幔子经过,这幔子就是他的身体。
21Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu.
21又有一位大祭司治理 神的家,
22Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.
22并我们心中天良的亏欠已经洒去,身体用清水洗净了,就当存着诚心和充足的信心来到 神面前;
23Tushikilie imara tumaini lile tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu.
23也要坚守我们所承认的指望,不至摇动,因为那应许我们的是信实的。
24Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema.
24又要彼此相顾,激发爱心,勉励行善。
25Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, Siku ile ya Bwana inakaribia.
25你们不可停止聚会,好像那些停止惯了的人,倒要彼此劝勉,既知道那日子临近,就更当如此。
26Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna dhabihu iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi.
26因为我们得知真道以后,若故意犯罪,赎罪的祭就再没有了;
27Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.
27惟有战惧等候审判和那烧灭众敌人的烈火。
28Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawa bila ya huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
28人干犯 摩西 的律法,凭两三个见证人,尚且不得怜恤而死,
29Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?
29何况人践踏 神的儿子,将那使他成圣之约的血当作平常,又亵慢施恩的 圣 灵,你们想,他要受的刑罚该怎样加重呢!
30Maana tunamfahamu yule aliyesema, “Mimi nitalipiza kisasi, mimi nitalipiza,” na ambaye alisema pia, “Bwana atawahukumu watu wake.”
30因为我们知道谁说:「伸冤在我,我必报应」;又 说 :「主要审判他的百姓。」
31Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!
31落在永生 神的手里,真是可怕的!
32Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, ninyi mlistahimili.
32你们要追念往日,蒙了光照以后所忍受大争战的各样苦难:
33Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo.
33一面被毁谤,遭患难,成了戏景,叫众人观看;一面陪伴那些受这样苦难的人。
34Mlishiriki mateso ya wafungwa, na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
34因为你们体恤了那些被捆锁的人,并且你们的家业被人抢去,也甘心忍受,知道自己有更美长存的家业。
35Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa.
35所以,你们不可丢弃勇敢的心;存这样的心必得大赏赐。
36Mnahitaji kuwa na uvumilivu, ili mweze kufanya anayotaka Mungu na kupokea kile alichoahidi.
36你们必须忍耐,使你们行完了 神的旨意,就可以得着所应许的。
37Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.
37因为还有一点点时候, 那要来的就来,并不迟延;
38Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi; walakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye.”
38只是义人必因信得生。 他若退后,我心里就不喜欢他。
39Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tunaamini na tunaokolewa.
39我们却不是退后入沉沦的那等人,乃是有信心以致灵魂得救的人。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.