马太福音 8
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1耶稣下了山,有许多人跟着他。
1Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata.
2有一个长大麻风的来拜他,说:「主若肯,必能叫我洁净了。」
2Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”
3耶稣伸手摸他,说:「我肯,你洁净了吧!」他的大麻风立刻就洁净了。
3Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, “Nataka! Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
4耶稣对他说:「你切不可告诉人,只要去把身体给祭司察看,献上 摩西 所吩咐的礼物,对众人作证据。」
4Kisha Yesu akamwambia, “Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
5耶稣进了 迦百农 ,有一个百夫长进前来,求他说:
5Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, ofisa mmoja Mroma alimwendea, akamsihi
6「主啊,我的仆人害瘫痪病,躺在家里,甚是疼苦。」
6akisema, “Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana.”
7耶稣说:「我去医治他。」
7Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.”
8百夫长回答说:「主啊,你到我舍下,我不敢当;只要你说一句话,我的仆人就必好了。
8Huyo ofisa akamwambia, “Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
9因为我在人的权下,也有兵在我以下;对这个说『去!』他就去;对那个说『来!』他就来;对我的仆人说:『你做这事!』他就去做。」
9Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda! naye huenda; na mwingine, Njoo! naye huja; na mtumishi wangu, Fanya kitu hiki! naye hufanya.”
10耶稣听见就希奇,对跟从的人说:「我实在告诉你们,这么大的信心,就是在 以色列 中,我也没有遇见过。
10Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii.
11我又告诉你们,从东从西,将有许多人来,在天国里与 亚伯拉罕 、 以撒 、 雅各 一同坐席;
11Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni.
12惟有本国的子民竟被赶到外边黑暗里去,在那里必要哀哭切齿了。」
12Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno.”
13耶稣对百夫长说:「你回去吧!照你的信心,给你成全了。」那时,他的仆人就好了。
13Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, “Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini.” Na mtumishi wake akapona saa ileile.
14耶稣到了 彼得 家里,见 彼得 的岳母害热病躺着。
14Yesu alifika nyumbani kwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, ana homa kali.
15耶稣把她的手一摸,热就退了;她就起来服事耶稣。
15Basi, Yesu akamgusa huyo mama mkono, na homa ikamwacha; akasimama, akamtumikia.
16到了晚上,有人带着许多被鬼附的来到耶稣跟前,他只用一句话就把鬼都赶出去,并且治好了一切有病的人。
16Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
17这是要应验先知 以赛亚 的话,说: 他代替我们的软弱, 担当我们的疾病。
17Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu.”
18耶稣见许多人围着他,就吩咐渡到那边去。
18Yesu alipoona kundi la watu limemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake waende ng'ambo ya ziwa.
19有一个文士来,对他说:「夫子,你无论往哪里去,我要跟从你。」
19Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, “Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako.”
20耶稣说:「狐狸有洞,天空的飞鸟有窝,人子却没有枕头的地方。」
20Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia.”
21又有一个门徒对耶稣说:「主啊,容我先回去埋葬我的父亲。」
21Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu.”
22耶稣说:「任凭死人埋葬他们的死人;你跟从我吧!」
22Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao.”
23耶稣上了船,门徒跟着他。
23Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye.
24海里忽然起了暴风,甚至船被波浪掩盖;耶稣却睡着了。
24Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi.
25门徒来叫醒了他,说:「主啊,救我们,我们丧命啦!」
25Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe, tunaangamia!”
26耶稣说:「你们这小信的人哪,为什么胆怯呢?」于是起来,斥责风和海,风和海就大大地平静了。
26Yesu akawaambia, “Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?” Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa.
27众人希奇,说:「这是怎样的人?连风和海也听从他了!」
27Watu wakashangaa, wakasema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!”
28耶稣既渡到那边去,来到 加大拉 人的地方,就有两个被鬼附的人从坟茔里出来迎着他,极其凶猛,甚至没有人能从那条路上经过。
28Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi, ng'ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita katika njia hiyo.
29他们喊着说:「 神的儿子,我们与你有什么相干?时候还没有到,你就上这里来叫我们受苦吗?」
29Nao wakaanza kupiga kelele, “Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?”
30离他们很远,有一大群猪吃食。
30Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa.
31鬼就央求耶稣,说:「若把我们赶出去,就打发我们进入猪群吧!」
31Basi, hao pepo wakamsihi, “Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale.”
32耶稣说:「去吧!」鬼就出来,进入猪群。全群忽然闯下山崖,投在海里淹死了。
32Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.
33放猪的就逃跑进城,将这一切事和被鬼附的人所遭遇的都告诉人。
33Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
34合城的人都出来迎见耶稣,既见了就央求他离开他们的境界。
34Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.