Matendo 6
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manung'uniko kati ya wanafunzi waliosema Kigiriki na wale waliosema Kiebrania. Wale waliosema Kigiriki walinung'unika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
1那时,门徒增多,有说希腊话的 犹太 人向 希伯来 人发怨言,因为在天天的供给上忽略了他们的寡妇。
2Kwa hiyo, mitume kumi na wawili waliita jumuiya yote ya wanafunzi, wakasema, “Si vizuri sisi tuache kulihubiri neno la Mungu ili tushughulikie ugawaji wa mahitaji.
2十二使徒叫众门徒来,对他们说:「我们撇下 神的道去管理饭食,原是不合宜的。
3Hivyo, ndugu zetu, chagueni miongoni mwenu watu saba wenye sifa njema, waliojawa na Roho na wenye hekima; nasi tutawakabidhi jukumu hilo.
3所以弟兄们,当从你们中间选出七个有好名声、被 圣 灵充满、智慧充足的人,我们就派他们管理这事。
4Sisi, lakini, tutashughulika na sala na kazi ya kuhubiri neno la Mungu.”
4但我们要专心以祈祷、传道为事。」
5Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujawa na Roho Mtakatifu, Filipo, Prokoro, Nikanora, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye hapo awali alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.
5大众都喜悦这话,就拣选了 司提反 ,乃是大有信心、圣灵充满的人,又拣选 腓利 、 伯罗哥罗 、 尼迦挪 、 提门 、 巴米拿 ,并进 犹太 教的 安提阿 人 尼哥拉 ,
6Wakawaweka mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono.
6叫他们站在使徒面前。使徒祷告了,就按手在他们头上。
7Neno la Mungu likazidi kuenea na idadi ya waumini huko Yerusalemu ikaongezeka zaidi, na kundi kubwa la makuhani wakaipokea imani.
7神的道兴旺起来;在 耶路撒冷 门徒数目加增的甚多,也有许多祭司信从了这道。
8Mungu alimjalia Stefano neema tele, akampa nguvu nyingi hata akawa anatenda miujiza na maajabu kati ya watu.
8司提反 满得恩惠、能力,在民间行了大奇事和神迹。
9Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
9当时有称 利百地拿 会堂的几个人,并有 古利奈 、 亚历山大 、 基利家 、 亚细亚 各处会堂的几个人,都起来和 司提反 辩论。
10Lakini hawakuweza kumshinda kwa sababu ya hekima yake na kwa sababu ya yule Roho aliyeongoza maneno yake.
10司提反 是以智慧和 圣 灵说话,众人敌挡不住,
11Kwa hiyo waliwahonga watu kadhaa waseme: “Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kumkashifu Mose na kumkashifu Mungu.”
11就买出人来说:「我们听见他说谤 摩西 和 神的话。」
12Kwa namna hiyo, waliwachochea watu, wazee na walimu wa Sheria. Basi, wakamjia Stefano, wakamkamata na kumleta mbele ya Baraza kuu.
12他们又耸动了百姓、长老,并文士,就忽然来捉拿他,把他带到公会去,
13Walileta Barazani mashahidi wa uongo ambao walisema, “Mtu huyu haachi kamwe kusema maneno ya kupakashifu mahali hapa patakatifu na Sheria ya Mose.
13设下假见证,说:「这个人说话,不住地糟践圣所和律法。
14Kwa maana tulikwisha msikia akisema eti huyo Yesu wa Nazareti atapaharibu kabisa mahali hapa na kufutilia mbali desturi zile tulizopokea kutoka kwa Mose.”
14我们曾听见他说,这 拿撒勒 人耶稣要毁坏此地,也要改变 摩西 所交给我们的规条。」
15Wote waliokuwa katika kile kikao cha Baraza walimkodolea macho Stefano, wakauona uso wake umekuwa kama wa malaika.
15在公会里坐着的人都定睛看他,见他的面貌,好像天使的面貌。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.