Matendo 23
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema, “Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele ya Mungu.”
1保羅 定睛看着公會的人,說:「弟兄們,我在上帝面前行事為人都是憑着良心,直到今日。」
2Hapo Kuhani Mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wampige kofi mdomoni.
2大祭司 亞拿尼亞 就吩咐旁邊站着的人打他的嘴。
3Basi, Paulo akamwambia, “Mungu mwenyewe atakupiga kofi wewe uliye kama ukuta uliopakwa chokaa! Unawezaje kukaa hapo ili unihukumu kisheria na huku wewe mwenyewe unaivunja Sheria kwa kuamuru nipigwe?”
3保羅 對他說:「你這粉飾的牆,上帝要打你!你坐堂為的是按律法審問我,你竟違背律法,吩咐人打我嗎?」
4Watu waliokuwa wamesimama pale wakamwambia Paulo, “Unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu!”
4站在旁邊的人說:「你辱罵上帝的大祭司嗎?」
5Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kama yeye ni Kuhani Mkuu. Maana Maandiko yasema hivi: Usiseme vibaya juu ya mtawala wa watu wako.”
5保羅 說:「弟兄們,我不曉得他是大祭司; 經上 記着說:『不可毀謗你百姓的官長。』」
6Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaaza sauti yake mbele ya Baraza: “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu watafufuka.”
6保羅 看出大眾一半是撒都該人,一半是法利賽人,就在公會中大聲說:「弟兄們,我是法利賽人,也是法利賽人的子孫。我現在受審問,是為盼望死人復活。」
7Baada ya kusema hivyo, mzozo mkali ulitokea kati ya Mafarisayo na Masadukayo na mkutano ukagawanyika sehemu mbili.
7說了這話,法利賽人和撒都該人就爭論起來,會眾分為兩黨。
8Kisa chenyewe kilikuwa hiki: Masadukayo hushikilia kwamba wafu hawafufuki, hakuna malaika, na roho nazo hazipo. Lakini Mafarisayo husadiki hayo yote matatu.
8因為撒都該人說,沒有復活,也沒有天使和鬼魂;法利賽人卻說,兩樣都有。
9Kelele ziliongezeka na baadhi ya walimu wa Sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”
9於是大大地喧嚷起來。有幾個法利賽黨的文士站起來爭辯說:「我們看不出這人有甚麼惡處,倘若有鬼魂或是天使對他說過話,怎麼樣呢?」
10Mzozo ulizidi kuwa mwingi hata mkuu wa jeshi akaogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipandevipande. Kwa hiyo, aliwaamuru askari wake kuingia kati ya lile kundi, wamtoe Paulo na kumrudisha ndani ya ngome.
10那時大起爭吵,千夫長恐怕 保羅 被他們扯碎了,就吩咐兵丁下去,把他從眾人當中搶出來,帶進營樓去。
11Usiku uliofuata, Bwana alisimama karibu na Paulo, akamwambia, “Jipe moyo! Umenishuhudia katika Yerusalemu, utafanya vivyo hivyo mjini Roma.”
11當夜,主站在 保羅 旁邊,說:「放心吧!你怎樣在 耶路撒冷 為我作見證,也必怎樣在 羅馬 為我 作見證。」
12Kulipokucha, Wayahudi walifanya kikao cha faragha. Wakala kiapo: “Hatutakula wala kunywa mpaka tutakapokuwa tumekwisha muua Paulo.”
12到了天亮, 猶太 人同謀起誓,說:「若不先殺 保羅 就不吃不喝。」
13Watu zaidi ya arobaini ndio waliokula njama kufanya hivyo.
13這樣同心起誓的有四十多人。
14Basi, walikwenda kwa makuhani wakuu na wazee, wakasema, “Sisi tumeapa kwamba hatutaonja chochote kwa vinywa vyetu mpaka hapo tutakapokuwa tumemuua Paulo.
14他們來見祭司長和長老,說:「我們已經起了一個大誓,若不先殺 保羅 就不吃甚麼。
15Sasa basi, ninyi pamoja na Baraza tumeni ujumbe kwa mkuu wa jeshi ili amlete Paulo kwenu mkijisingizia kwamba mnataka kupata habari kamili zaidi juu yake. Tuko tayari kumuua hata kabla hajafika karibu.”
15現在你們和公會要知會千夫長,叫他帶下 保羅 到你們這裏來,假作要詳細察考他的事;我們已經預備好了,不等他來到跟前就殺他。」
16Lakini mtoto wa kiume wa dada yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.
16保羅 的外甥聽見他們設下埋伏,就來到營樓裏告訴 保羅 。
17Hapo Paulo akamwita mmoja wa askari, akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwa mkuu wa jeshi; ana kitu cha kumwambia.”
17保羅 請一個百夫長來,說:「你領這少年人去見千夫長,他有事告訴他。」
18Askari akamchukua huyo kijana, akamwongoza mpaka kwa mkuu wa jeshi, akasema, “Yule mfungwa Paulo ameniita akaniomba nimlete kijana huyu kwako kwa maana ana jambo la kukwambia.”
18於是把他領去見千夫長,說:「被囚的 保羅 請我到他那裏,求我領這少年人來見你;他有事告訴你。」
19Mkuu wa jeshi alimshika huyo kijana mkono, akampeleka mahali pa faragha, akamwuliza, “Una nini cha kuniambia?”
19千夫長就拉着他的手,走到一旁,私下問他說:「你有甚麼事告訴我呢?」
20Yeye akasema, “Wayahudi wamepatana wakuombe umpeleke Paulo Barazani wakijisingizia kwamba Baraza lingependa kupata habari kamili zaidi juu yake.
20他說:「 猶太 人已經約定,要求你明天帶下 保羅 到公會裏去,假作要詳細查問他的事。
21Lakini wewe usikubali kwa maana kuna watu zaidi ya arobaini walio tayari kumvamia. Wameapa kutokula wala kunywa mpaka watakapokuwa wamemuua. Sasa wako tayari, wanangojea tu uamuzi wako.”
21你切不要隨從他們;因為他們有四十多人埋伏,已經起誓說,若不先殺 保羅 就不吃不喝。現在預備好了,只等你應允。」
22Mkuu wa jeshi alimwacha aende zake akimwonya asimwambie mtu yeyote kwamba amemletea habari hizo.
22於是千夫長打發少年人走,囑咐他說:「不要告訴人你將這事報給我了。」
23Basi, mkuu wa jeshi aliwaita askari wawili akawaambia, “Wekeni tayari askari mia mbili, wapanda farasi sabini na askari mia mbili wa mikuki, waende Kaisarea; muwe tayari kuondoka kabla ya saa tatu leo usiku.
23千夫長便叫了兩個百夫長來,說:「預備步兵二百,馬兵七十,長槍手二百,今夜亥初往 凱撒利亞 去;
24Wekeni farasi kadhaa kwa ajili ya Paulo; mfikisheni salama kwa Felisi, mkuu wa mkoa.”
24也要預備牲口叫 保羅 騎上,護送到巡撫 腓力斯 那裏去。」
25Halafu mkuu huyo wa jeshi akaandika barua hivi:
25千夫長又寫了文書,
26“Mimi Klaudio Lusia ninakuandikia wewe Mheshimiwa Felisi, mkuu wa mkoa. Salamu!
26大略說:「 克勞第‧呂西亞 ,請巡撫 腓力斯 大人安。
27“Wayahudi walimkamata mtu huyu na karibu wangemuua kama nisingalifahamishwa kwamba yeye ni raia wa Roma na hivyo nikaenda pamoja na askari nikamwokoa.
27這人被 猶太 人拿住,將要殺害,我得知他是 羅馬 人,就帶兵丁下去救他出來。
28Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao.
28因要知道他們告他的緣故,我就帶他下到他們的公會去,
29Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za Sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
29便查知他被告是因他們律法的辯論,並沒有甚麼該死該綁的罪名。
30Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumuua, niliamua kumleta kwako. Nikamwambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”
30後來有人把要害他的計謀告訴我,我就立時解他到你那裏去,又吩咐告他的人在你面前告他。」
31Basi, hao askari walimchukua Paulo kama walivyoamriwa; wakampeleka usiku uleule mpaka Antipatri.
31於是,兵丁照所吩咐他們的,將 保羅 夜裏帶到 安提帕底 。
32Kesho yake askari wa miguu walirudi ngomeni, wakawaacha wale askari wapanda farasi waendelee na safari pamoja na Paulo.
32第二天,讓馬兵護送,他們就回營樓去。
33Walipofika Kaisarea walimpa mkuu wa mkoa ile barua na kumweka Paulo chini ya mamlaka yake.
33馬兵來到 凱撒利亞 ,把文書呈給巡撫,便叫 保羅 站在他面前。
34Felisi alipoisoma hiyo barua aliwauliza Paulo ametoka mkoa gani. Alipofahamishwa kwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia,
34巡撫看了文書,問 保羅 是哪省的人,既曉得他是 基利家 人,
35akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
35就說:「等告你的人來到,我要細聽你的事」;便吩咐人把他看守在 希律 的衙門裏。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.