2 Wakorintho 2
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
1Basi nimeamua nisiwatembelee tena kuwatia huzuni.
1我自己定了主意再到你們那裏去,必須大家沒有憂愁。
2Maana nikiwahuzunisha ninyi, basi, ni nani atakayenifariji? Ni walewale niliowahuzunisha!
2倘若我叫你們憂愁,除了我叫那憂愁的人以外,誰能叫我快樂呢?
3Ndiyo maana niliwaandikia—sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na ninyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba, mimi nikifurahi, ninyi nyote pia mnafurahi.
3我曾把這事寫給你們,恐怕我到的時候,應該叫我快樂的那些人,反倒叫我憂愁。我也深信,你們眾人都以我的快樂為自己的快樂。
4Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwaonyesheni kwamba nawapenda mno.
4我先前心裏難過痛苦,多多地流淚,寫信給你們,不是叫你們憂愁,乃是叫你們知道我格外地疼愛你們。
5Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi—ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.
5若有叫人憂愁的,他不但叫我憂愁,也是叫你們眾人有幾分憂愁。我說幾分,恐怕說得太重。
6Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.
6這樣的人受了眾人的責罰也就夠了,
7Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.
7倒不如赦免他,安慰他,免得他憂愁太過,甚至沉淪了。
8Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda.
8所以我勸你們,要向他顯出堅定不移的愛心來。
9Madhumuni yangu kuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kama mko tayari kutii katika kila jambo.
9為此我先前也寫信給你們,要試驗你們,看你們凡事順從不順從。
10Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe—kama kweli ninacho cha kusamehe—nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,
10你們赦免誰,我也赦免誰。我若有所赦免的,是在基督面前為你們赦免的,
11ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo.
11免得撒但趁着機會勝過我們,因我們並非不曉得他的詭計。
12Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nilikuta mlango u wazi kwa ajili ya kazi ya Bwana.
12我從前為基督的福音到了 特羅亞 ,主也給我開了門。
13Lakini nilifadhaika sana kwa kutomkuta ndugu yetu Tito. Ndiyo maana niliwaaga wote pale nikaenda Makedonia.
13那時,因為沒有遇見兄弟 提多 ,我心裏不安,便辭別那裏的人往 馬其頓 去了。
14Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali.
14感謝上帝!常率領我們在基督裏誇勝,並藉着我們在各處顯揚那因認識基督而有的香氣。
15Maana sisi ni kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristo anamtolea Mungu, harufu nzuri inayofikia wote wanaookolewa na wanaopotea.
15因為我們在上帝面前,無論在得救的人身上或滅亡的人身上,都有基督馨香之氣。
16Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi ya namna hiyo?
16在這等人,就作了死的香氣叫他死;在那等人,就作了活的香氣叫他活。這事誰能當得起呢?
17Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.
17我們不像那許多人,為利混亂上帝的道;乃是由於誠實,由於上帝,在上帝面前憑着基督講道。
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.