约翰福音 13
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1逾越节以前,耶稣知道自己离世归父的时候到了。他既然爱世间属自己的人,就爱他们到底。
1Ilikuwa kabla ya sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
2吃晚饭的时候,魔鬼已将卖耶稣的意思放在 西门 的儿子 加略 人 犹大 心里。
2Basi, Yesu na wanafunzi wake walikuwa mezani kwa chakula cha jioni. Ibilisi alikwisha mtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, nia ya kumsaliti Yesu.
3耶稣知道父已将万有交在他手里,且知道自己是从 神出来的,又要归到 神那里去,
3Yesu alijua kwamba Baba alikuwa amemkabidhi kila kitu, na kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwa Mungu.
4就离席站起来,脱了衣服,拿一条手巾束腰,
4Basi, Yesu aliondoka mezani, akaweka kando vazi lake, akachukua kitambaa na kujifunga kiunoni.
5随后把水倒在盆里,就洗门徒的脚,并用自己所束的手巾擦干。
5Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuipangusa kwa kile kitambaa alichojifungia.
6挨到 西门·彼得 , 彼得 对他说:「主啊,你洗我的脚吗?」
6Basi, akamfikia Simoni Petro; naye Petro akasema, “Bwana, wewe utaniosha miguu mimi?”
7耶稣回答说:「我所做的,你如今不知道,后来必明白。」
7Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.”
8彼得 说:「你永不可洗我的脚!」耶稣说:「我若不洗你,你就与我无分了。」
8Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
9西门·彼得 说:「主啊,不但我的脚,连手和头也要洗。」
9Simoni Petro akamwambia, “Bwana, nioshe, si miguu tu, bali na mikono yangu na kichwa pia.”
10耶稣说:「凡洗过澡的人,只要把脚一洗,全身就干净了。你们是干净的,然而不都是干净的。」
10Yesu akamwambia, “Aliyekwisha oga hana lazima ya kunawa isipokuwa miguu, maana amekwisha takata mwili wote. Ninyi mmetakata, lakini si nyote.”
11耶稣原知道要卖他的是谁,所以说:「你们不都是干净的。」
11(Yesu alimjua yule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema: “Ninyi mmetakata, lakini si nyote.”)
12耶稣洗完了他们的脚,就穿上衣服,又坐下,对他们说:「我向你们所做的,你们明白吗?
12Alipokwisha waosha miguu na kuvaa tena vazi lake, aliketi mezani, akawaambia, “Je, mmeelewa hayo niliyowatendeeni?
13你们称呼我夫子,称呼我主,你们说的不错,我本来是。
13Ninyi mwaniita Mwalimu na Bwana, nanyi mwasema vyema, kwa kuwa ndimi.
14我是你们的主,你们的夫子,尚且洗你们的脚,你们也当彼此洗脚。
14Basi, ikiwa mimi niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha ninyi miguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.
15我给你们作了榜样,叫你们照着我向你们所做的去做。
15Nimewapeni mfano, ili nanyi pia mfanye kama nilivyowafanyieni.
16我实实在在地告诉你们,仆人不能大于主人,差人也不能大于差他的人。
16Kweli nawaambieni, mtumishi si mkuu zaidi kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu zaidi kuliko yule aliyemtuma.
17你们既知道这事,若是去行就有福了。
17Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza.
18我这话不是指着你们众人说的,我知道我所拣选的是谁。现在要应验经上的话,说:『同我吃饭的人用脚踢我。』
18“Haya nisemayo hayawahusu ninyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.
19如今事情还没有成就,我要先告诉你们,叫你们到事情成就的时候可以信我是 基督 。
19Mimi nimewaambieni mambo haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini kuwa mimi ndimi.
20我实实在在地告诉你们,有人接待我所差遣的,就是接待我;接待我,就是接待那差遣我的。」
20Kweli nawaambieni anayempokea yule ninayemtuma anaponipokea mimi; na anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma.”
21耶稣说了这话,心里忧愁,就明说:「我实实在在地告诉你们,你们中间有一个人要卖我了。」
21Alipokwisha sema hayo, Yesu alifadhaika sana rohoni, akasema wazi, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu atanisaliti!”
22门徒彼此对看,猜不透所说的是谁。
22Wanafunzi wakatazama wasiweze kabisa kujua anasema nani.
23有一个门徒,是耶稣所爱的,侧身挨近耶稣的怀里。
23Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana, alikuwa ameketi karibu na Yesu.
24西门·彼得 点头对他说:「你告诉我们,主是指着谁说的。」
24Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: “Mwulize anasema juu ya nani.”
25那门徒便就势靠着耶稣的胸膛,问他说:「主啊,是谁呢?」
25Mwanafunzi huyo akasogea karibu zaidi na Yesu, akamwuliza, “Bwana, ni nani?”
26耶稣回答说:「我蘸一点饼给谁,就是谁。」耶稣就蘸了一点饼,递给 加略 人 西门 的儿子 犹大 。
26Yesu akajibu, “Yule nitakayempa kipande cha mkate nilichochovya katika sahani, ndiye.” Basi, akatwaa kipande cha mkate, akakichovya katika sahani, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti.
27他吃了以后,撒但就入了他的心。耶稣便对他说:「你所做的,快做吧!」
27Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia. Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanye haraka!”
28同席的人没有一个知道是为什么对他说这话。
28Lakini hakuna hata mmoja wa wale waliokaa pale mezani aliyefahamu kwa nini alikuwa amemwambia hivyo.
29有人因 犹大 带着钱囊,以为耶稣是对他说:「你去买我们过节所应用的东西」,或是叫他拿什么周济穷人。
29Kwa kuwa Yuda alikuwa na wajibu wa kuutunza mfuko wa fedha, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini.
30犹大 受了那点饼,立刻就出去。那时候是夜间了。
30Basi, Yuda alipokwisha twaa kile kipande cha mkate, akatoka nje mara. Na ilikuwa usiku.
31他既出去,耶稣就说:「如今人子得了荣耀, 神在人子身上也得了荣耀。
31Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Mtu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake.
32神要因自己荣耀人子,并且要快快地荣耀他。
32Na kama utukufu wa Mungu umefunuliwa ndani ya Mwana, basi, naye Mungu ataudhihirisha utukufu wa Mwana ndani yake mwenyewe, na atafanya hivyo mara.
33小子们,我还有不多的时候与你们同在;后来你们要找我,但我所去的地方你们不能到。这话我曾对 犹太 人说过,如今也照样对你们说。
33“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: Niendako ninyi hamwezi kwenda!
34我赐给你们一条新命令,乃是叫你们彼此相爱;我怎样爱你们,你们也要怎样相爱。
34Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda ninyi.
35你们若有彼此相爱的心,众人因此就认出你们是我的门徒了。」
35Mkipendana, watu wote watajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu.”
36西门·彼得 问耶稣说:「主往哪里去?」耶稣回答说:「我所去的地方,你现在不能跟我去,后来却要跟我去。」
36Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Niendako huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.”
37彼得 说:「主啊,我为什么现在不能跟你去?我愿意为你舍命!」
37Petro akamwambia “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajili yako!”
38耶稣说:「你愿意为我舍命吗?我实实在在地告诉你,鸡叫以先,你要三次不认我。」
38Yesu akajibu, “Je, uko tayari kweli kufa kwa ajili yangu? Kweli nakwambia, kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu!”
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.