约翰福音 18
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1耶稣说了这话,就同门徒出去,过了 汲沦溪 。在那里有一个园子,他和门徒进去了。
1Yesu alipokwisha sema hayo, alikwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, pamoja na wanafunzi wake. Mahali hapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingia humo pamoja na wanafunzi wake.
2卖耶稣的 犹大 也知道那地方,因为耶稣和门徒屡次上那里去聚集。
2Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
3犹大 领了一队兵,和祭司长并法利赛人的差役,拿着灯笼、火把、兵器,就来到园里。
3Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
4耶稣知道将要临到自己的一切事,就出来对他们说:「你们找谁?」
4Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, “Mnamtafuta nani?”
5他们回答说:「找 拿撒勒 人耶稣。」耶稣说:「我就是!」卖他的 犹大 也同他们站在那里。
5Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
6耶稣一说「我就是」,他们就退后倒在地上。
6Basi, Yesu alipowaambia: “Mimi ndiye”, wakarudi nyuma, wakaanguka chini.
7他又问他们说:「你们找谁?」他们说:「找 拿撒勒 人耶稣。」
7Yesu akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!”
8耶稣说:「我已经告诉你们,我就是。你们若找我,就让这些人去吧。」
8Yesu akawaambia, “Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.”
9这要应验耶稣从前的话,说:「你所赐给我的人,我没有失落一个。」
9(Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.”)
10西门·彼得 带着一把刀,就拔出来,将大祭司的仆人砍了一刀,削掉他的右耳;那仆人名叫 马勒古 。
10Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
11耶稣就对 彼得 说:「收刀入鞘吧,我父所给我的那杯,我岂可不喝呢?」
11Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipa Baba?”
12那队兵和千夫长,并 犹太 人的差役就拿住耶稣,把他捆绑了,
12Kile kikosi cha askari, mkuu wake na walinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga
13先带到 亚那 面前,因为 亚那 是本年作大祭司 该亚法 的岳父。
13na kumpeleka kwanza kwa Anasi; Anasi alikuwa baba mkwe wa Kayafa ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo.
14这 该亚法 就是从前向 犹太 人发议论说「一个人替百姓死是有益的」那位。
14Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudi kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa.
15西门·彼得 跟着耶稣,还有一个门徒跟着。那门徒是大祭司所认识的,他就同耶稣进了大祭司的院子。
15Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu.
16彼得 却站在门外。大祭司所认识的那个门徒出来,和看门的使女说了一声,就领 彼得 进去。
16Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngoja mlango, akamwingiza Petro ndani.
17那看门的使女对 彼得 说:「你不也是这人的门徒吗?」他说:「我不是。」
17Huyo msichana mngoja mlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
18仆人和差役因为天冷,就生了炭火,站在那里烤火; 彼得 也同他们站着烤火。
18Watumishi na walinzi walikuwa wamewasha moto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawa wanaota moto. Naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
19大祭司就以耶稣的门徒和他的教训盘问他。
19Basi, Kuhani akamwuliza Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
20耶稣回答说:「我从来是明明地对世人说话。我常在会堂和殿里,就是 犹太 人聚集的地方教训人;我在暗地里并没有说什么。
20Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na Hekaluni, mahali wakutanikiapo Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
21你为什么问我呢?可以问那听见的人,我对他们说的是什么;我所说的,他们都知道。」
21Kwa nini waniuliza mimi? Waulize wale waliosikia nini niliwaambia. Wao wanajua nilivyosema.”
22耶稣说了这话,旁边站着的一个差役用手掌打他,说:「你这样回答大祭司吗?」
22Alipokwisha sema hayo mlinzi mmoja aliyekuwa amesimama hapo akampiga kofi akisema, “Je, ndivyo unavyomjibu Kuhani Mkuu?”
23耶稣说:「我若说的不是,你可以指证那不是;我若说的是,你为什么打我呢?」
23Yesu akamjibu, “Kama nimesema vibaya, onyesha huo ubaya; lakini ikiwa nimesema vema, mbona wanipiga?”
24亚那 就把耶稣解到大祭司 该亚法 那里,仍是捆着解去的。
24Basi, Anasi akampeleka Yesu akiwa amefungwa, kwa Kuhani Mkuu Kayafa.
25西门·彼得 正站着烤火,有人对他说:「你不也是他的门徒吗?」 彼得 不承认,说:「我不是。」
25Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
26有大祭司的一个仆人,是 彼得 削掉耳朵那人的亲属,说:「我不是看见你同他在园子里吗?」
26Mmoja wa watumishi wa Kuhani Mkuu, jamaa wa yule aliyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, “Je, mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?”
27彼得 又不承认。立时鸡就叫了。
27Petro akakana tena; mara jogoo akawika.
28众人将耶稣从 该亚法 那里往衙门内解去,那时天还早。他们自己却不进衙门,恐怕染了污秽,不能吃逾越 节的筵席 。
28Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa najisi.
29彼拉多 就出来,到他们那里,说:「你们告这人是为什么事呢?」
29Kwa hiyo, Pilato aliwaendea nje, akasema, “Mna mashtaka gani juu ya mtu huyu?”
30他们回答说:「这人若不是作恶的,我们就不把他交给你。」
30Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.”
31彼拉多 说:「你们自己带他去,按着你们的律法审问他吧。」 犹太 人说:「我们没有杀人的权柄。」
31Pilato akawaambia, “Haya, mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kufuatana na Sheria yenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote.”
32这要应验耶稣所说自己将要怎样死的话了。
32(Ilifanyika hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonyesha atakufa kifo gani.)
33彼拉多 又进了衙门,叫耶稣来,对他说:「你是 犹太 人的王吗?」
33Pilato akaingia tena ndani ya ikulu, akamwita Yesu na kumwuliza: “Ati wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”
34耶稣回答说:「这话是你自己说的,还是别人论我对你说的呢?」
34Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekwambia habari zangu?”
35彼拉多 说:「我岂是 犹太 人呢?你本国的人和祭司长把你交给我。你做了什么事呢?」
35Pilato akamjibu, “Je, ni Myahudi mimi? Taifa lako na makuhani wamekuleta kwangu. Umefanya nini?”
36耶稣回答说:「我的国不属这世界;我的国若属这世界,我的臣仆必要争战,使我不至于被交给 犹太 人。只是我的国不属这世界。」
36Yesu akamjibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu watumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa.”
37彼拉多 就对他说:「这样,你是王吗?」耶稣回答说:「你说我是王。我为此而生,也为此来到世间,特为给真理作见证。凡属真理的人就听我的话。」
37Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
38彼拉多 说:「真理是什么呢?」 说了这话,又出来到 犹太 人那里,对他们说:「我查不出他有什么罪来。
38Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake.
39但你们有个规矩,在逾越节要我给你们释放一个人,你们要我给你们释放 犹太 人的王吗?」
39Lakini, mnayo desturi kwamba mimi niwafungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Basi, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?”
40他们又喊着说:「不要这人,要 巴拉巴 !」这 巴拉巴 是个强盗。
40Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.