Mathayo 3
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chamorro: Gospels, Acts and Psalms
1Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:
1AYO sija na jaane, mato si Juan Bautista ya sumetmon gui desierton Judea,
2“Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
2Ylegña: Fanmañotsot sa y raenon langet jumijijot.
3Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake.”
3Sa esta güiya uje y guinin jasangan y profeta Isaias, na ilegña: Inagang ni umagang gui desierto: Famauleg y chalan y Señot, natunas y chalanña.
4Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
4Y magaguña si Juan y pilon cameyo yan y godeña cuero na jachaflileg gui senturaña, ya y naña y apacha sija yan y miet jalom tano.
5Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
5Ayo nae mapos malag para güiya, Jerusalem yan Judea yan todo y tano gui oriyan Jordan,
6wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
6Ya esta manmatagpange pot güiya, guiya Jordan, jasangan claro y isaoñija.
7Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
7Ya jalie megae na Fariseo yan Saduseo sija na manmamaela para y tinagpangeña ya ilegña: Rasan culebla, jaye jamyo fumanagüe na insujaye y binibo ni mamaela?
8Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
8Fanmamatinas tinegcha digno ni y sinetsot.
9Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, Baba yetu ni Abrahamu! Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
9Ya chamiyo jumajaso sumangan gui sanjalommiyo, na si Abraham tatata; ya guajo sumangane jamyo, na siña si Yuus janacajulo este sija na acho famaguon gui as Abraham.
10Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
10Pago, esta locue y gachae gaegue na mapolo gui jale y trongcon jayo sija; ya todo y trongcon jayo ni ti manogcha mauleg, umautut ya umapolo gui guafe.
11Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
11Guajo magajet jutagpange jamyo nu y janom para minañotsot, lao y mamamaela gui tateco, mas guaja ninasiñaña qui guajo: y sapatosña ti mauleg yo na jupula; güiya infantinagpange ni Espiritu Santo yan y guafe.
12Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
12Y abanicoña gaegue gui canaeña, ya unagasgas y tablaña, ya unaetnon y triguña jalom gui jalom camalin, ya usonggue y pajan trigo gui taejinecog na guafe.
13Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
13Anae mato si Jesus guinin Galilea, malag Jordan gui as Juan para utinagpange.
14Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, “Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe.”
14Lao si Juan ti malago, ilegña: Nesesita yo matagpange pot jago, enaojao na mamaela guiya guajo?
15Lakini Yesu akamjibu, “Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka.” Hapo Yohane akakubali.
15Inepe as Jesus ilegña: Diejaloja, sa taegüenao mauleg para utacumple y todo na tininas. Ayo nae pinelo.
16Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake.
16Ya si Jesus, anae munjayan matagpange, cajulo gusisija guine y janom, y langet mababa pot güiya ya malie y Espiritun Yuus tumunog calang paluma y sumaga gui jiloña.
17Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye.”
17Ya estagüe, un vos guinin y langet na ilegña: Estagüiya y lajijo ni y guefyajo.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.