马可福音 15
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1一到早晨,祭司长和长老、文士、全公会的人大家商议,就把耶稣捆绑,解去交给 彼拉多 。
1Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
2彼拉多 问他说:「你是 犹太 人的王吗?」耶稣回答说:「你说的是。」
2Pilato akamwuliza Yesu, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
3祭司长告他许多的事。
3Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
4彼拉多 又问他说:「你看,他们告你这么多的事,你什么都不回答吗?」
4Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako.”
5耶稣仍不回答,以致 彼拉多 觉得希奇。
5Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
6每逢这节期,巡抚照众人所求的,释放一个囚犯给他们。
6Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
7有一个人名叫 巴拉巴 ,和作乱的人一同捆绑。他们作乱的时候,曾杀过人。
7Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
8众人上去求巡抚,照常例给他们办。
8Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
9彼拉多 说:「你们要我释放 犹太 人的王给你们吗?」
9Pilato akawauliza, “Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?”
10他原晓得,祭司长是因为嫉妒才把耶稣解了来。
10Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
11只是祭司长挑唆众人,宁可释放 巴拉巴 给他们。
11Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
12彼拉多 又说:「那么样,你们所称为 犹太 人的王,我怎么办他呢?」
12Pilato akawauliza tena, “Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”
13他们又喊着说:「把他钉十字架!」
13Watu wote wakapaaza sauti tena: “Msulubishe!”
14彼拉多 说:「为什么呢?他做了什么恶事呢?」他们便极力地喊着说:「把他钉十字架!」
14Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, “Msulubishe!”
15彼拉多 要叫众人喜悦,就释放 巴拉巴 给他们,将耶稣鞭打了,交给人钉十字架。
15Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
16兵丁把耶稣带进衙门院里,叫齐了全营的兵。
16Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
17他们给他穿上紫袍,又用荆棘编做冠冕给他戴上,
17Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
18就庆贺他说:「恭喜, 犹太 人的王啊!」
18Wakaanza kumsalimu, “Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!”
19又拿一根苇子打他的头,吐唾沫在他脸上,屈膝拜他。
19Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
20戏弄完了,就给他脱了紫袍,仍穿上他自己的衣服,带他出去,要钉十字架。
20Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
21有一个 古利奈 人 西门 ,就是 亚历山大 和 鲁孚 的父亲,从乡下来,经过那地方,他们就勉强他同去,好背着耶稣的十字架。
21Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
22他们带耶稣到了 各各他 地方( 各各他 翻出来就是髑髅地),
22Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu la Kichwa.”
23拿没药调和的酒给耶稣,他却不受。
23Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
24于是将他钉在十字架上,拈阄分他的衣服,看是谁得什么。
24Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
25钉他在十字架上是巳初的时候。
25Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
26在上面有他的罪状,写的是:「 犹太 人的王。」
26Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: “Mfalme wa Wayahudi.”
27他们又把两个强盗和他同钉十字架,一个在右边,一个在左边。
27Pamoja naye waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
no verse 28 in this text
28Hapo yakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, “Aliwekwa kundi moja na waovu.”
29从那里经过的人辱骂他,摇着头说:「咳!你这拆毁圣殿、三日又建造起来的,
29Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
30可以救自己,从十字架上下来吧!」
30Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!”
31祭司长和文士也是这样戏弄他,彼此说:「他救了别人,不能救自己。
31Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
32以色列 的王基督,现在可以从十字架上下来,叫我们看见,就信了。」那和他同钉的人也是讥诮他。
32Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
33从午正到申初,遍地都黑暗了。
33Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
34申初的时候,耶稣大声喊着说:「以罗伊!以罗伊!拉马撒巴各大尼?」(翻出来就是:我的 神!我的 神!为什么离弃我?)
34Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
35旁边站着的人,有的听见就说:「看哪,他叫 以利亚 呢!」
35Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, “Sikiliza! Anamwita Eliya!”
36有一个人跑去,把海绒蘸满了醋,绑在苇子上,送给他喝,说:「且等着,看 以利亚 来不来把他取下。」
36Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!”
37耶稣大声喊叫,气就断了。
37Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
38殿里的幔子从上到下裂为两半。
38Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
39对面站着的百夫长看见耶稣这样喊叫断气,就说:「这人真是 神的儿子!」
39Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40还有些妇女远远地观看;内中有 抹大拉 的 马利亚 ,又有小 雅各 和 约西 的母亲 马利亚 ,并有 撒罗米 ,
40Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
41就是耶稣在 加利利 的时候,跟随他、服事他的那些人,还有同耶稣上 耶路撒冷 的好些妇女 在那里观看 。
41Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
42到了晚上,因为这是预备日,就是安息日的前一日,
42Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
43有 亚利马太 的 约瑟 前来,他是尊贵的议士,也是等候 神国的。他放胆进去见 彼拉多 ,求耶稣的身体;
43Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
44彼拉多 诧异耶稣已经死了,便叫百夫长来,问他耶稣死了久不久。
44Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
45既从百夫长得知实情,就把耶稣的尸首赐给 约瑟 。
45Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
46约瑟 买了细麻布,把耶稣取下来,用细麻布裹好,安放在磐石中凿出来的坟墓里,又滚过一块石头来挡住墓门。
46Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
47抹大拉 的 马利亚 和 约西 的母亲 马利亚 都看见安放他的地方。
47Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.