马可福音 13
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1耶稣从殿里出来的时候,有一个门徒对他说:「夫子,请看,这是何等的石头!何等的殿宇!」
1Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
2耶稣对他说:「你看见这大殿宇吗?将来在这里没有一块石头留在石头上,不被拆毁了。」
2Yesu akamwambia, “Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa.”
3耶稣在 橄榄山 上对 圣 殿而坐。 彼得 、 雅各 、 约翰 ,和 安得烈 暗暗地问他说:
3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
4「请告诉我们,什么时候有这些事呢?这一切事将成的时候有什么预兆呢?」
4“Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?”
5耶稣说:「你们要谨慎,免得有人迷惑你们。
5Yesu akaanza kuwaambia, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
6将来有好些人冒我的名来,说:『我是 基督 』,并且要迷惑许多人。
6Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.
7你们听见打仗和打仗的风声,不要惊慌。 这些事 是必须有的,只是末期还没有到。
7Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
8民要攻打民,国要攻打国;多处必有地震、饥荒。这都是灾难的起头。
8Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
9但你们要谨慎;因为人要把你们交给公会,并且你们在会堂里要受鞭打,又为我的缘故站在诸侯与君王面前,对他们作见证。
9“Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
10然而,福音必须先传给万民。
10Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
11人把你们拉去交官的时候,不要预先思虑说什么;到那时候,赐给你们什么话,你们就说什么;因为说话的不是你们,乃是圣灵。
11Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
12弟兄要把弟兄,父亲要把儿子,送到死地;儿女要起来与父母为敌,害死他们;
12Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
13并且你们要为我的名被众人恨恶。惟有忍耐到底的,必然得救。」
13Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14「你们看见那行毁坏可憎的,站在不当站的地方(读 这经 的人须要会意)。那时,在 犹太 的,应当逃到山上;
14“Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
15在房上的,不要下来,也不要进去拿家里的东西;
15Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
16在田里的,也不要回去取衣裳。
16Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
17当那些日子,怀孕的和奶孩子的有祸了!
17Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
18你们应当祈求,叫这些事不在冬天临到。
18Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
19因为在那些日子必有灾难,自从 神创造万物直到如今,并没有这样的灾难,后来也必没有。
19Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
20若不是主减少那日子,凡有血气的,总没有一个得救的;只是为主的选民,他将那日子减少了。
20Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
21那时若有人对你们说:『看哪,基督在这里』,或说:『基督在那里』,你们不要信!
21“Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
22因为假基督、假先知将要起来,显神迹奇事,倘若能行,就把选民迷惑了。
22Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
23你们要谨慎。看哪,凡事我都预先告诉你们了。」
23Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
24「在那些日子,那灾难以后, 日头要变黑了, 月亮也不放光,
24“Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
25众星要从天上坠落, 天势都要震动。
25Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
26那时,他们要看见人子有大能力、大荣耀,驾云降临。
26Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
27他要差遣天使,把他的选民,从四方,从地极直到天边,都招聚了来。」
27Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
28「你们可以从无花果树学个比方:当树枝发嫩长叶的时候,你们就知道夏天近了。
28“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
29这样,你们几时看见这些事成就,也该知道人子近了,正在门口了。
29Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
30我实在告诉你们,这世代还没有过去,这些事都要成就。
30Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
31天地要废去,我的话却不能废去。」
31Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
32「但那日子,那时辰,没有人知道,连天上的使者也不知道,子也不知道,惟有父知道。
32“Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
33你们要谨慎,警醒祈祷,因为你们不晓得那日期几时来到。
33Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
34这事正如一个人离开本家,寄居外邦,把权柄交给仆人,分派各人当做的工,又吩咐看门的警醒。
34Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
35所以,你们要警醒;因为你们不知道家主什么时候来,或晚上,或半夜,或鸡叫,或早晨;
35Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
36恐怕他忽然来到,看见你们睡着了。
36Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
37我对你们所说的话,也是对众人说:要警醒!」
37Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!”
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.