雅各书 2
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1我的弟兄们,你们信奉我们荣耀的主耶稣基督,便不可按着外貌待人。
1Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.
2若有一个人带着金戒指,穿着华美衣服,进你们的会堂去;又有一个穷人穿着肮脏衣服也进去;
2Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi machafu.
3你们就重看那穿华美衣服的人,说:「请坐在这好位上」;又对那穷人说:「你站在那里」,或「坐在我脚凳下边。」
3Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,”
4这岂不是你们偏心待人,用恶意断定人吗?
4je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya?
5我亲爱的弟兄们,请听, 神岂不是拣选了世上的贫穷人,叫他们在信上富足,并承受他所应许给那些爱他之人的国吗?
5Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea Utawala aliowaahidia wale wanaompenda.
6你们反倒羞辱贫穷人。那富足人岂不是欺压你们、拉你们到公堂去吗?
6Lakini ninyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamizeni na kuwapeleka mahakamani?
7他们不是亵渎你们所敬奉的尊名吗?
7Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa?
8经上记着说:「要爱人如己。」你们若全守这至尊的律法才是好的。
8Kama mnaitimiza ile sheria ya Utawala kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Mpende binadamu mwenzako kama unavyojipenda wewe mwenyewe”, mtakuwa mnafanya vema kabisa.
9但你们若按外貌待人,便是犯罪,被律法定为犯法的。
9Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheria inawahukumu ninyi kuwa mna hatia.
10因为凡遵守全律法的,只在一条上跌倒,他就是犯了众条。
10Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja Sheria yote.
11原来那说「不可奸淫」的,也说「不可杀人」;你就是不奸淫,却杀人,仍是成了犯律法的。
11Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue”. Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.
12你们既然要按 使人 自由的律法受审判,就该照这律法说话行事。
12Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.
13因为那不怜悯人的,也要受无怜悯的审判;怜悯原是向审判夸胜。
13Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma. Lakini huruma hushinda hukumu.
14我的弟兄们,若有人说自己有信心,却没有行为,有什么益处呢?这信心能救他吗?
14Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa?
15若是弟兄或是姊妹,赤身露体,又缺了日用的饮食;
15Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula.
16你们中间有人对他们说:「平平安安地去吧!愿你们穿得暖,吃得饱」,却不给他们身体所需用的,这有什么益处呢?
16Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
17这样,信心若没有行为就是死的。
17Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
18必有人说:「你有信心,我有行为;你将你没有行为的信心指给我看,我便借着我的行为,将我的信心指给你看。」
18Lakini mtu anaweza kusema: “Wewe unayo imani, mimi ninayo matendo!” Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
19你信 神只有一位,你信的不错;鬼魔也信,却是战惊。
19Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.
20虚浮的人哪,你愿意知道没有行为的信心是死的吗?
20Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo imekufa?
21我们的祖宗 亚伯拉罕 把他儿子 以撒 献在坛上,岂不是因行为称义吗?
21Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu.
22可见,信心是与他的行为并行,而且信心因着行为才得成全。
22Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani yake ilikamilishwa kwa matendo yake.
23这就应验经上所说:「 亚伯拉罕 信 神,这就算为他的义。」他又得称为 神的朋友。
23Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu.”
24这样看来,人称义是因着行为,不是单因着信。
24Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake na si kwa imani peke yake.
25妓女 喇合 接待使者,又放他们从别的路上出去,不也是一样因行为称义吗?
25Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
26身体没有灵魂是死的,信心没有行为也是死的。
26Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.