Ufunuo 2
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Chinese Union Version, punctuated (Simplified)
1“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu.
1「你要写信给 以弗所 教会的使者,说:『那右手拿着七星、在七个金灯台中间行走的,说:
2Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.
2我知道你的行为、劳碌、忍耐,也知道你不能容忍恶人。你也曾试验那自称为使徒却不是使徒的,看出他们是假的来。
3Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo.
3你也能忍耐,曾为我的名劳苦,并不乏倦。
4Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
4然而有一件事我要责备你,就是你把起初的爱心离弃了。
5Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako mahali pake.
5所以,应当回想你是从哪里坠落的,并要悔改,行起初所行的事。你若不悔改,我就临到你那里,把你的灯台从原处挪去。
6Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
6然而你还有一件可取的事,就是你恨恶 尼哥拉 一党人的行为,这也是我所恨恶的。
7“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu.
7圣 灵向众教会所说的话,凡有耳的,就应当听!得胜的,我必将 神乐园中生命树的果子赐给他吃。』」
8“Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi: “Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho, ambaye alikufa na akaishi tena.
8「你要写信给 士每拿 教会的使者,说:『那首先的、末后的、死过又活的,说:
9Najua taabu zako; najua pia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri; najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.
9我知道你的患难,你的贫穷(你却是富足的),也知道那自称是 犹太 人所说的毁谤话,其实他们不是 犹太 人,乃是撒但一会的人。
10Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa, nami nitawapeni taji ya uzima.
10你将要受的苦你不用怕。魔鬼要把你们中间几个人下在监里,叫你们被试炼,你们必受患难十日。你务要至死忠心,我就赐给你那生命的冠冕。
11“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
11圣 灵向众教会所说的话,凡有耳的,就应当听!得胜的,必不受第二次死的害。』」
12“Kwa malaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: “Huu ndio ujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.
12「你要写信给 别迦摩 教会的使者,说:『那有两刃利剑的,说:
13Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.
13我知道你的居所,就是有撒但座位之处;当我忠心的见证人 安提帕 在你们中间、撒但所住的地方被杀之时,你还坚守我的名,没有弃绝我的道。
14Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi.
14然而,有几件事我要责备你:因为在你那里有人服从了 巴兰 的教训;这 巴兰 曾教导 巴勒 将绊脚石放在 以色列 人面前,叫他们吃祭偶像之物,行奸淫的事。
15Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
15你那里也有人照样服从了 尼哥拉 一党人的教训。
16Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
16所以,你当悔改;若不悔改,我就快临到你那里,用我口中的剑攻击他们。
17“Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.
17圣 灵向众教会所说的话,凡有耳的,就应当听!得胜的,我必将那隐藏的吗哪赐给他,并赐他一块白石,石上写着新名;除了那领受的以外,没有人能认识。』」
18“Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
18「你要写信给 推雅推喇 教会的使者,说:『那眼目如火焰、脚像光明铜的 神之子说:
19Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
19我知道你的行为、爱心、信心、勤劳、忍耐,又知道你末后所行的 善 事,比起初所行的更多。
20Lakini nina hoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamke Yezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu.
20然而,有一件事我要责备你,就是你容让那自称是先知的妇人 耶洗别 教导我的仆人,引诱他们行奸淫,吃祭偶像之物。
21Nimempa muda wa kutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.
21我曾给她悔改的机会,她却不肯悔改她的淫行。
22Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeye pamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa na mateso makali. Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubu matendo yao mabaya waliyotenda naye.
22看哪,我要叫她病卧在床。那些与她行淫的人,若不悔改所行的,我也要叫他们同受大患难。
23Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
23我又要杀死她的党类,叫众教会知道,我是那察看人肺腑心肠的,并要照你们的行为报应你们各人。
24“Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
24至于你们 推雅推喇 其余的人,就是一切不从那教训、不晓得他们素常所说撒但深奥之理的人,我告诉你们,我不将别的担子放在你们身上。
25Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
25但你们已经有的,总要持守,直等到我来。
26“Wanaoshinda, na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa.
26那得胜又遵守我命令到底的,我要赐给他权柄制伏列国;
27Naam, nitawapa uwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani, watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuyavunjavunja kama chombo cha udongo.
27他必用铁杖辖管他们,将他们如同窑户的瓦器打得粉碎,像我从我父领受的权柄一样。
28Tena nitawapa nyota ya asubuhi.
28我又要把晨星赐给他。
29“Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
29圣 灵向众教会所说的话,凡有耳的,就应当听!』」
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.