Mathayo 26
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
Berean Standard Bible
1Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,
1When Jesus had finished saying all these things, He told His disciples,
2“Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”
2“You know that the Passover is two days away, and the Son of Man will be handed over to be crucified.”
3Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, Kuhani Mkuu.
3At that time the chief priests and elders of the people assembled in the courtyard of the high priest, whose name was Caiaphas,
4Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.
4and they conspired to arrest Jesus covertly and kill Him.
5Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
5“But not during the feast,” they said, “or there may be a riot among the people.”
6Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,
6While Jesus was in Bethany in the home of Simon the Leper,
7mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.
7a woman came to Him with an alabaster jar of expensive perfume, which she poured on His head as He reclined at the table.
8Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?
8When the disciples saw this, they were indignant and asked, “Why this waste?
9Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha.”
9This perfume could have been sold at a high price, and the money given to the poor.”
10Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.
10Aware of this, Jesus asked, “Why are you bothering this woman? She has done a beautiful deed to Me.
11Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.
11The poor you will always have with you, but you will not always have Me.
12Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.
12By pouring this perfume on Me, she has prepared My body for burial.
13Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”
13Truly I tell you, wherever this gospel is preached in all the world, what she has done will also be told in memory of her.”
14Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu,
14Then one of the Twelve, the one called Judas Iscariot, went to the chief priests
15akawaambia, “Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?” Wakamhesabia sarafu thelathini za fedha;
15and asked, “What are you willing to give me if I hand Him over to you?” And they set out for him thirty pieces of silver.
16na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.
16So from then on Judas looked for an opportunity to betray Jesus.
17Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
17On the first day of the Feast of Unleavened Bread, the disciples came to Jesus and asked, “Where do You want us to prepare for You to eat the Passover?”
18Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie: Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.”
18He answered, “Go into the city to a certain man and tell him that the Teacher says, ‘My time is near. I will keep the Passover with My disciples at your house.’”
19Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka.
19So the disciples did as Jesus had directed them and prepared the Passover.
20Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili.
20When evening came, Jesus was reclining with the twelve disciples.
21Walipokuwa wakila, Yesu akasema, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.”
21And while they were eating, He said to them, “Truly I tell you, one of you will betray Me.”
22Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja, “Bwana! Je, ni mimi?”
22They were deeply grieved and began to ask Him one after another, “Surely not I, Lord?”
23Yesu akajibu, “Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti.
23Jesus answered, “The one who has dipped his hand into the bowl with Me will betray Me.
24Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa.”
24The Son of Man will go just as it is written about Him, but woe to that man by whom He is betrayed. It would be better for him if he had not been born.”
25Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, “Mwalimu! Je, ni mimi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.”
25Then Judas, who would betray Him, said, “Surely not I, Rabbi?” Jesus answered, “You have said it yourself.”
26Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, “Twaeni mle; huu ni mwili wangu.”
26While they were eating, Jesus took bread, spoke a blessing and broke it, and gave it to the disciples, saying, “Take and eat; this is My body.”
27Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema, “Nyweni nyote;
27Then He took the cup, gave thanks, and gave it to them, saying, “Drink from it, all of you.
28maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi.
28This is My blood of the covenant, which is poured out for many for the forgiveness of sins.
29Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
29I tell you, I will not drink of this fruit of the vine from now on until that day when I drink it anew with you in My Father’s kingdom.”
30Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.
30And when they had sung a hymn, they went out to the Mount of Olives.
31Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.
31Then Jesus said to them, “This very night you will all fall away on account of Me. For it is written: ‘I will strike the Shepherd, and the sheep of the flock will be scattered.’
32Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya.”
32But after I have risen, I will go ahead of you into Galilee.”
33Petro akamwambia Yesu “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe.”
33Peter said to Him, “Even if all fall away on account of You, I never will.”
34Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
34“Truly I tell you,” Jesus declared, “this very night, before the rooster crows, you will deny Me three times.”
35Petro akamwambia, “Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.
35Peter replied, “Even if I have to die with You, I will never deny You.” And all the other disciples said the same thing.
36Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali.”
36At that time Jesus went with His disciples to a place called Gethsemane, and He told them, “Sit here while I go over there and pray.”
37Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko.
37He took with Him Peter and the two sons of Zebedee and began to be sorrowful and deeply distressed.
38Hapo akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
38Then He said to them, “My soul is consumed with sorrow to the point of death. Stay here and keep watch with Me.”
39Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: “Baba yangu, kama inawezekana, aacha kikombe hiki cha mateso kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe.”
39Going a little farther, He fell facedown and prayed, “My Father, if it is possible, let this cup pass from Me. Yet not as I will, but as You will.”
40Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
40Then Jesus returned to the disciples and found them sleeping. “Were you not able to keep watch with Me for one hour?” He asked Peter.
41Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu.”
41“Watch and pray so that you will not enter into temptation. For the spirit is willing, but the body is weak.”
42Akaenda tena mara ya pili akasali: “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako yafanyike.”
42A second time He went away and prayed, “My Father, if this cup cannot pass unless I drink it, may Your will be done.”
43Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi.
43And again Jesus returned and found them sleeping—for their eyes were heavy.
44Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno yaleyale.
44So He left them and went away once more and prayed a third time, saying the same thing.
45Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, “Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi.
45Then He returned to the disciples and said, “Are you still sleeping and resting? Look, the hour is near, and the Son of Man is betrayed into the hands of sinners.
46Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti.”
46Rise, let us go! See, My betrayer is approaching!”
47Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao, mara akaja Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili. Pamoja naye walikuja watu wengi wenye mapanga na marungu ambao walitumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
47While Jesus was still speaking, Judas, one of the Twelve, arrived, accompanied by a large crowd armed with swords and clubs, sent from the chief priests and elders of the people.
48Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: “Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni.”
48Now the betrayer had arranged a signal with them: “The One I kiss is the man; arrest Him.”
49Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, “Shikamoo, Mwalimu!” Kisha akambusu.
49Going directly to Jesus, he said, “Greetings, Rabbi!” and kissed Him.
50Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya ulichokuja kufanya.” Hapo wale watu wakaja, wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni.
50“Friend,” Jesus replied, “do what you came for.” Then the men stepped forward, seized Jesus, and arrested Him.
51Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono, akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.
51At this, one of Jesus’ companions drew his sword and struck the servant of the high priest, cutting off his ear.
52Hapo Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako alani, maana yeyote anayeutumia upanga, atakufa kwa upanga.
52“Put your sword back in its place,” Jesus said to him. “For all who draw the sword will die by the sword.
53Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
53Are you not aware that I can call on My Father, and He will at once put at My disposal more than twelve legions of angels?
54Lakini yatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayo kwamba ndivyo inavyopaswa kuwa?”
54But how then would the Scriptures be fulfilled that say it must happen this way?”
55Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, “Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata!
55At that time Jesus said to the crowd, “Have you come out with swords and clubs to arrest Me as you would an outlaw? Every day I sat teaching in the temple courts, and you did not arrest Me.
56Lakini haya yote yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie.” Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
56But this has all happened so that the writings of the prophets would be fulfilled.” Then all the disciples deserted Him and fled.
57Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu wa Sheria na wazee.
57Those who had arrested Jesus led Him away to the house of Caiaphas the high priest, where the scribes and elders had gathered.
58Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa.
58But Peter followed Him at a distance, right up to the courtyard of the high priest. And he went in and sat down with the guards to see the outcome.
59Basi, makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu wapate kumwua,
59Now the chief priests and the whole Sanhedrin were seeking false testimony against Jesus in order to put Him to death.
60lakini hawakupata ushahidi wowote, ingawa walikuja mashahidi wengi wa uongo. Mwishowe wakaja mashahidi wawili,
60But they did not find any, though many false witnesses came forward. Finally two came forward
61wakasema, “Mtu huyu alisema: Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.”
61and declared, “This man said, ‘I am able to destroy the temple of God and rebuild it in three days.’”
62Kuhani Mkuu akasimama, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”
62So the high priest stood up and asked Him, “Have You no answer? What are these men testifying against You?”
63Lakini Yesu akakaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!”
63But Jesus remained silent. Then the high priest said to Him, “I charge You under oath by the living God: Tell us if You are the Christ, the Son of God.”
64Yesu akamwambia, “Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu sasa mtamwona Mwana wa Mtu ameketi upande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
64“You have said it yourself,” Jesus answered. “But I say to all of you, from now on you will see the Son of Man sitting at the right hand of Power and coming on the clouds of heaven.”
65Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake.
65At this, the high priest tore his clothes and declared, “He has blasphemed! Why do we need any more witnesses? Look, now you have heard the blasphemy.
66Ninyi mwaonaje?” Wao wakamjibu, “Anastahili kufa!”
66What do you think?” “He deserves to die,” they answered.
67Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi,
67Then they spit in His face and struck Him. Others slapped Him
68wakasema, “Haya Kristo, tutabirie; ni nani amekupiga!”
68and said, “Prophesy to us, Christ! Who hit You?”
69Petro alikuwa ameketi nje uani. Basi, mtumishi mmoja wa kike akamwendea, akasema, “Wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”
69Meanwhile, Peter was sitting out in the courtyard, and a servant girl came up to him. “You also were with Jesus the Galilean,” she said.
70Petro akakana mbele ya wote akisema, “Sijui hata unasema nini.”
70But he denied it before them all: “I do not know what you are talking about.”
71Alipokuwa akitoka mlangoni, mtumishi mwingine wa kike akamwona, akawaambia wale waliokuwa pale, “Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.”
71When Peter had gone out to the gateway, another servant girl saw him and said to the people there, “This man was with Jesus of Nazareth.”
72Petro akakana tena kwa kiapo: “Simjui mtu huyo.”
72And again he denied it with an oath: “I do not know the man!”
73Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”
73After a little while, those standing nearby came up to Peter. “Surely you are one of them,” they said, “for your accent gives you away.”
74Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, “Simjui mtu huyo!” Mara jogoo akawika.
74At that he began to curse and swear to them, “I do not know the man!” And immediately a rooster crowed.
75Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Basi, akatoka nje akalia sana.
75Then Peter remembered the word that Jesus had spoken: “Before the rooster crows, you will deny Me three times.” And he went outside and wept bitterly.
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.