馬可福音 7
Chinese Union Version, punctuated (Traditional)
Biblia Takatifu (Swahili): New Testament portions
1有法利賽人和幾個文士從 耶路撒冷 來,到耶穌那裏聚集。
1Baadhi ya Mafarisayo na walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu.
2他們曾看見他的門徒中有人用俗手,就是沒有洗的手,吃飯。(
2Waliona kwamba baadhi ya wanafunzi wake walikula mikate kwa mikono najisi, yaani bila kunawa.
3原來法利賽人和 猶太 人都拘守古人的遺傳,若不仔細洗手就不吃飯;
3Maana Mafarisayo na Wayahudi wengine wote huzingatia mapokeo ya wazee wao: hawali kitu kabla ya kunawa mikono ipasavyo.
4從市上來,若不洗浴也不吃飯;還有好些別的規矩,他們歷代拘守,就是洗杯、罐、銅器 等物 。)
4Tena hawali kitu chochote kutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
5法利賽人和文士問他說:「你的門徒為甚麼不照古人的遺傳,用俗手吃飯呢?」
5Basi, Mafarisayo na walimu wa Sheria wakamwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawayajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu, bali hula chakula kwa mikono najisi?”
6耶穌說:「 以賽亞 指着你們假冒為善之人所說的預言是不錯的。如經上說: 這百姓用嘴唇尊敬我, 心卻遠離我。
6Yesu akawajibu, “Wanafiki ninyi! Nabii Isaya alitabiri ukweli juu yenu alipoandika: Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno matupu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
7他們將人的吩咐當作道理教導人, 所以拜我也是枉然。
7Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.
8你們是離棄上帝的誡命,拘守人的遺傳」;
8Ninyi mnaiacha amri ya Mungu na kushikilia maagizo ya watu.”
9又說:「你們誠然是廢棄上帝的誡命,要守自己的遺傳。
9Yesu akaendelea kusema, “Ninyi mnajua kuepa kwa ujanja sheria ya Mungu kwa ajili ya kufuata mapokeo yenu.
10摩西 說:『當孝敬父母』;又說:『咒罵父母的,必治死他。』
10Maana Mose aliamuru: Waheshimu baba yako na mama yako, na, Anayemlaani baba au mama, lazima afe.
11你們倒說:『人若對父母說:我所當奉給你的,已經作了各耳板』(各耳板就是供獻的意思),
11Lakini ninyi mwafundisha, Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani ni zawadi kwa Mungu),
12以後你們就不容他再奉養父母。
12basi, halazimiki tena kuwasaidia wazazi wake.
13這就是你們承接遺傳,廢了上帝的道。你們還做許多這樣的事。」
13Hivyo ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa ajili ya mafundisho mnayopokezana. Tena mnafanya mambo mengi ya namna hiyo.”
14耶穌又叫眾人來,對他們說:「你們都要聽我的話,也要明白。
14Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe.
15從外面進去的不能污穢人,惟有從裏面出來的乃能污穢人。」
15Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu toka nje ambacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakini kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia mtu najisi.”
no verse 16 in this text
16Mwenye masikio na asikie!
17耶穌離開眾人,進了屋子,門徒就問他這比喻的意思。
17Alipouacha umati wa watu na kuingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza maana ya huo mfano.
18耶穌對他們說:「你們也是這樣不明白嗎?豈不曉得凡從外面進入的,不能污穢人,
18Naye akawaambia, “Je, hata ninyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu toka nje hakiwezi kumtia unajisi,
19因為不是入他的心,乃是入他的肚腹,又落到茅廁裏( 這是說 ,各樣的食物都是潔淨的)」;
19kwa maana hakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?” (Kwa kusema hivyo, Yesu alivihalalisha vyakula vyote.)
20又說:「從人裏面出來的,那才能污穢人;
20Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.
21因為從裏面,就是從人心裏,發出惡念、苟合、
21Kwa maana kutoka ndani, katika moyo wa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji,
22偷盜、凶殺、姦淫、貪婪、邪惡、詭詐、淫蕩、嫉妒、謗讟、驕傲、狂妄。
22uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu.
23這一切的惡都是從裏面出來,且能污穢人。」
23Maovu hayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu najisi.”
24耶穌從那裏起身,往 泰爾 、 西頓 的境內去,進了一家,不願意人知道,卻隱藏不住。
24Yesu aliondoka hapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
25當下,有一個婦人,她的小女兒被污鬼附着,聽見耶穌的事,就來俯伏在他腳前。
25Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
26這婦人是 希臘 人,屬 敘利腓尼基 族。她求耶穌趕出那鬼離開她的女兒。
26Mama huyo alikuwa Mgiriki, mwenyeji wa Sirofoinike. Basi, akamwomba Yesu amtoe binti yake pepo mchafu.
27耶穌對她說:「讓兒女們先吃飽,不好拿兒女的餅丟給狗吃。」
27Yesu akamwambia, “Kwanza watoto washibe; kwa maana si vizuri kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”
28婦人回答說:「主啊,不錯;但是狗在桌子底下也吃孩子們的碎渣兒。」
28Lakini huyo mama akasema, “Sawa, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”
29耶穌對她說:「因這句話,你回去吧;鬼已經離開你的女兒了。」
29Yesu akamwambia, “Kwa sababu ya neno hilo, nenda. Pepo amemtoka binti yako!”
30她就回家去,見小孩子躺在床上,鬼已經出去了。
30Basi, akaenda nyumbani kwake, akamkuta mtoto amelala kitandani, na pepo amekwisha mtoka.
31耶穌又離了 泰爾 的境界,經過 西頓 ,就從 低加坡里 境內來到 加利利 海 。
31Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
32有人帶着一個耳聾舌結的人來見耶穌,求他按手在他身上。
32Basi, wakamletea bubu-kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
33耶穌領他離開眾人,到一邊去,就用指頭探他的耳朵,吐唾沫抹他的舌頭,
33Yesu akamtenga na umati wa watu, akamtia vidole masikioni, akatema mate na kumgusa ulimi.
34望天歎息,對他說:「以法大!」就是說:「開了吧!」
34Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, “Efatha,” maana yake, “Funguka.”
35他的耳朵就開了,舌結也解了,說話也清楚了。
35Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukafunguliwa, akaanza kusema sawasawa.
36耶穌囑咐他們不要告訴人;但他越發囑咐,他們越發傳揚開了。
36Yesu akawaamuru wasimwambie mtu juu ya jambo hilo. Lakini kadiri alivyowakataza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari hiyo.
37眾人分外希奇,說:「他所做的事都好,他連聾子也叫他們聽見,啞巴也叫他們說話。」
37Watu walishangaa sana, wakasema, “Amefanya yote vyema: amewajalia viziwi kusikia, na bubu kusema!”
Tip: use the ← and → keys to turn chapters.